Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Nyololo Animal Gift Project pamoja na wananchi wakicheza ngoma ya asili ya wahehe.
Na Fredy Mgunda,Iringa
JUMLA ya wananchi 3600
wanategemea kunufaika na mradi wa Nyololo Animal Gift Project unaofadhiliwa na
world vision Marekani na kutekelezwa na world vision Tanzania wilayani Mufindi
mkoani Iringa wenye lengo la kuinua Kipato na kuboresha maisha ya wananchi.
Akizungumza wakati wa kuzindua
mradi huo,meneja wa kanda ya Iringa wa world vision Tanzania Vicent Kasuga
alisema kuwa mradi huo utaghalimu kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kwa wananchi
wa vijiji saba (7) vya wilaya ya Mufindi
Mkoani Iringa.
Kasuga alisema kuwa lengo la
mradi huo ni kuboresha mnyololo wa thamani kwa kutoa aina tatu (3) za mifugo
ambazo ni Ng’ombe wa Maziwa,kuku na Nguruwe na aina mbalimbali ya mazao ya
bustani kwa ajili ya uboreshaji wa lishe kupitia makundi ya mbogamboga na
matunda kama vile Parachichi,pasheni,chainizi,karoti,kabeji,Nyanya chungu,Hoho
na kadharika.
Alisema kuwa kiasi hicho cha
fedha kitatumika kununua Ng’ombe wa maziwa mia tatu (300),Nguruwe 600 na kuku
400 kwa kipindi chote cha mradi na watu 1200 wanatarajiwa kunufaika moja kwa
moja na wengine 2400 (indirect Participants) watanuafaika na mradi huo.
Kasuga alisema kuwa mradi huo
utashirikisha wataalamu wa kilimo na mifugo,viongozi wa serikali ngazi ya kata
na vijiji kuwatambua wanufaika wa mradi ambao watakuwa na sifa ya kusimamia na
kuendesha miradi ya ufugaji wa Ng’ombe,kuku na Nguruwe kwa kuzingatia vigezo
vitakavyowekwa.
Aidha Kasuga alisema kuwa mradi huo lazima
ujenge misingi bora ya kuinua kipato kwa kushirikiana na serikali na wadau
wengine,kwa kuhakikisha mchango kwenye ulinzi wa mtoto kwa kupunguza ama kuondoa
kabisa kunyanyaswa kwa watoto.
“Tumekuwa na mkakati wa kimataifa
kwenye jambo la ukatili kwa watoto,hasa ndoa za utotoni kwa kuwa umekuwa
ukatili unaofanywa kwa muda mrefu sasa,watoto wengi wamekuwa wanatumikishwa na
kuasahau shule ni lazima tutokomeze ukatili dhidi ya watoto,” alisema Kasuga
Katika wilaya ya Mufindi shirika
la World Vision Tanzania limeanza kufanya kazi rasmi mwaka jana (2021) likiwa
na jumla ya miradi ya maendeleo yaani Area Programms 3 mmojawapo ni huu wa Nyololo
ambao unatekeleza miradi ya maji,Usafi,Afya,Lishe,Elimu na uongezaji wa kipato.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wananchi na wanufaika wa miradi ya World
Vision Tanzania wanapaswa kutoa ushirkiano wa kutosha na kuitunza miradi ili
kuleta manufaa kwa wananchi wote.
Mtambule alisema kuwa mradi huo
unakwenda kutatua tatizo la lishe kwa wananchi wa wilaya hiyo na kuwaondolea
udumavu ambao umekuwa unawatesa sana wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa mwananchi yoyote
atakae jitokeza kuuharibu mradi huo serikali itawachukulia hatua kali za
kisheria ili kudhibiti uharibifu wa miradi na kusaidia wananchi kunufaika na
mradio huo.
Naye meneja wa shamba la mifugo
Sao Hill Thomas Tegulo alisema kuwa Ng’ombe hao watasaidia kuinua kipato cha
wananchi kwa kuwa wanyama hao wanatunzwa kwa viwango vya kimataifa hivyo
wanufaika watapata Ng’ombe bora ambae atakupa faida kubwa.
Tengalo alisema kuwa wamekuwa
wanauzoefu wa kufuga wanyama hao kwa ubora unaotakiwa kwa kufanya mnyama huyo
kutoa maziwa mengi ambayo yatakuwa na faida kwa wananchi ambao wanafuga wanyama
hao.