Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kuzindua Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma .
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, akizungumza katika uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika leo April 6,2022 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu,akizungumza katika uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika leo April 6,2022 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose, akizungumza katika uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika leo April 6,2022 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi, akizungumza katika uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika leo April 6,2022 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa M-MAMA Bi. Dolorosa Duncan kuhusu Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA kabla ya kuuzindua katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza jambo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimpongeza Msanii Christian Bella kwenye uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma .
Mkururugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa akimtunza Msanii Christian Bella wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park leo Jijini Dodoma.
Mkururugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mha. Kundo Mathew na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Sitholizwe Mdlalose na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Group Mwamvita Makamba wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park leo Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma .
…………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua Mfumo wa kielektroniki wa Kitaifa wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga.
Pia ameitaka Wizara ya habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari kukamilisha haraka iwezekanavyo mpango wa sheria za kulinda taarifa binafsi mtandaoni.
Rais Samia amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua mfumo wa usafirishaji wa dharura wa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) iliyoratibiwa na kampuni ya simu ya Vodacom katika viwanja vya Chinangali.
Rais Samia amesema lengo la mfumo huo ni kuhakikisha kuwa wakina mama zaidi ya milioni moja ambao ni walengwa wanafikiwa na kunufaika na huduma hii katika kipindi cha miaka mitano.
‘Amesema tangu kuanza kwa majaribio ya mfumo wa M-MAMA katika Wilaya ya Sengerema na mkoani Shinyanga mwaka 2013, wanawake na watoto 12,000 wameshahudumiwa na hivyo kusaidia kupunguza vifo vya kina mama vinavyotokana na ukosefu wa usafiri.”amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia ameitaka kampuni ya Vodacom kuufanya mfumo huo uwe endelevu na uwafikie wananchi wengi na kutoa wito kwa kampuni zingine zilizopo nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Rais Samia amesema, pamoja na jitihada zilizofanywa na Serikali, bado zipo changamoto ambazo husababisha vifo vya mama na mtoto kabla au baada ya kujifungua kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya haraka na usafiri wa uhakika wa kumwahisha mama mjamzito kufika katika kituo cha afya.
Pamoja kuanzishwa kwa mfumo huo wa M-mama RAIS Samia amesema serikali itaendelea kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na magari ya kubeba wagonjwa angalau kila kata gari moja.
“Tumeagiza ‘ambulance’ 233 za kawaida ambazo zitamwangwa Tanzania nzima lakini pia tumeagiza ‘ambulance’ 25 ambazo ni ‘advance’ hizi ni kama ngazi ya rufani kama zile zinakuwa hazitoshi au hazina vifaa basi hizi 25 zitatumika lakini pia tumeagiza magari 242 ya uratibu ,
Nimatuini yangu kwamba magari na ambulance hizi zitakwenda kuongeza nguvu kwenye huu mpango wa m-mama ili kuwawahisha watoto na kina mama mahospitalini”amesema
Rais Samia pia ameiagiza Wizara ya Afya kufanya haraka kuiangalia mifumo inayotumiwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD) hasa katika mfumo wa ufuatiliaji dawa tangu inapotoka hadi pale inapomfika kwenye vituo.
Rais Samia amewaagiza Wakuu wa Mikoa katika Halmashauri ambazo mfumo wa M-MAMA utatekelezwa, kutenga fedha zitakazoongeza nguvu kwenye huduma ya mama na mtoto mchanga.