Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko Mwalimu Commercial Bank Bi.Leticia Ndongole akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam.Mshauri wa Mwalimu Commercial Bank katika masuala ya kutoa mikopo na huduma za fedha kwa Taasisi za Elimu Bw.Issa Ngwegwe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya Institute of Heavy Equipment and Technology (IEHT),Mhandisi Edwin Godwin akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo cha Covenant Institute of Accountancy and Technology(CIAT) Bw.Godson Mkaro akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Vyuo vya City College of Health and Allied Sciences Tanzania Bw.Shabani Mwanga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam.
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KATIKA jiitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye kukuza sekta ya Elimu kwa ujumla, Mwalimu Benki wameanzisha bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko Mwalimu Commercial Bank Bi.Leticia Ndongole amesema kuwa bidhaa hiyo ni ya mkopo wa muda mfupi unaofanikisha kulipa ada ya mwaka mzima na hivyo kumfanya mzazi?mwanafunzi kusoma kwa utulivu.
Aidha Bi.Leticia amesema wameingia mikataba na wamiliki wa mashule mbalimbali ili kutoa mikopo ya masharti nafuu kuunga juhudi za Serikali katika kuinua Elimu pamoja na stadi za ujuzi kupitia vyuo mbalimbali.
“Wabia wetu katika bidhaa hii OPPORTUNITY EDU FINANCE ambao wameiongezea thamani bidhaa hii ambapo watajikita kuwajengea uwezo wamiliki wa mashule ili mikopo hii iwe na tija”. Amesema
Pamoja na hayo amezitaja shule na vyuo ambavyo tayari wanamikataba kwa ajili ya kuwakopesha wazazi/wanafunzi ADA CHAP CHAP navyo ni Eagles High School-Bagamoyo, City College of Health and Allied Sciences Kampasi ya Ilala na Goba (Mount Ukombozi), Covenant Institute of Accountancy and Technology-Kurasini, Covenant Financial Consults kwa wanataaluma wa uhasibu yaani CPA na Institute of Heavy Equipment and Technology-Kijitonyama hivyo basi Mwalimu Commercial Bank inaendelea kupokea wabia wengine wamiliki wa shule na vyuo ili kuweza kuwafikia wahitaji wengi>
Kwa upande wake Mshauri wa Mwalimu Commercial Bank katika masuala ya kutoa mikopo na huduma za fedha kwa Taasisi za Elimu Bw.Issa Ngwegwe amesema wameamua kusaidia benki hiyo kuhakikisha inajikita zaidi kuangalia sekta ya elimu kama sekta kwa ujumla hivyo wameanza na bidhaa hiyo ya ADA CHAP CHAP lakini kuna mambo mengine yatataraji yanayyiohusiana na mikopo pamoja huduma zingine za kifedha katika Taasisi za Elimu.
Nae Mkurugenzi wa Vyuo vya City College of Health and Allied Sciences Tanzania Bw.Shabani Mwanga amesema kumekuwa na upungufu wa wanafunzi kufika vyuoni kutokana ukosefu wa ada ambayo ingemsaidia kuendelea na masomo hivyo kupitia ADA CHAP CHAP itarahisha kwa wanafunzi kupata ada na kuendelea kusoma bila wasiwasi.
“Jambo hili limekuwa kubwa na sisi kama Taasisi tumekuuwa tukitafuta huku na kule ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia wanafunzi lakini kupitia Mwalimu Commercial Bank nadhani suruhisho limepatikana”. Amesema Bw.Mwanga.