Mkuu wa wilaya yaTabora mjini Dkt Yahya Nawanda akitoa nasaha kwa Emmanuel Ntonge
MBUNGE wa jimbo la Tabora mjini Emmanuel Adamson Mwakasaka Mwenye kipara akiwa na mstaafu wa shule ya sekondari Milambo wavulana Emmanuele Ntonge aliyevaa kofia nyekundu wakisakata rumba
***********************
Na Lucas Raphael,Tabora
MBUNGE wa jimbo la Tabora mjini Emmanuel Adamson Mwakasaka amesema kustaafu utumishi wa umma au serikalini siyo mwisho wa maisha au kifo bali ni wajibu wa kisheria na unatakiwa kujipongeza kwa utumishi uliotukuka hadi kufikia hatua hiyo.
Mwakasaka alisema hayo kwenye hafla ya kumpongeza Emmanuel Alex Ntonge kwenye ukumbi wa Ntonge Hall baada ya ksstaafu katika shule ya sekondari ya wavulana Milambo akiwa idara ya uhasibu.
Mbunge huyo wa jimbo la Tabora mjini aliongeza kuwa Ntonge wanafahamiana vyema na kwamba wakiwa vijana walishawahi kuwa marafiki na ni mtumishi mwenye weledi na maarifa mazuri akiwa kazini.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Dkt Yahya Nawanda alimtaja mstaafu Emmanuel Ntonge ni mstaafu aliyependa kushirikiana na watu katika kufanya kazi zake kwa weledi na uangalifu mkubwa ili asiende kinyume na taratibu,kanuni ma sheria.
Naye mstaafu wa shule ya sekondari Milambo wavulana Emmanuele Ntonge alishukuru kumaliza muda wake salama na anapenda mambo ya kijamii na licha ya kustaafu ataendelea kutumika kushauri kwa manufaa ya mkoa wa Tabora.
Ntonge aliongeza kuwa amestaaafu kwa mujibu wa sheria na kustaafu ni njia ya kujifunza mengi zaidi ya na yeye sasa anageukia suala la ufugaji na kilimo ili aendelee na maisha bora na salama.
Alisema uzee mara nyingi ni hofu wakati mwingine unapostaafu unapoteza marafiki wengi na katika kustaafu lazima ujiandaae na maisha mapya ya uzeeni kwani ni zamu ya watoto na watumishi walioko kazini.
Aliongeza kuwa na kutoa mfano siku zote gari bovu huvutwa na gari zima na anawashukuru viongozi walipo kama mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Dkt Yahaya Nawanda,mkuu wa wilaya ya Kaliua Poul Chacha na mkurugenzi wa shirika la maji safi na maji taka Tabora Mayunga Kashilimu..
Alitaja wengine kuwa ni diwani wa kata Gongoni Kessy Sharif,mstahiki Meya Tabora Ramadhan Kapera,diwani mwenyeji wa kata ya Mtendeni Yahya Mhamali na wageni wengine waliopo.
Akiishukuru kwa niaba ya familia Alex Ntonge ambaye ni mtumishi idara ya fedha shirika la maji safi na maji taka Tabora (TUWASA) akiwa meneja wa fedha,alisema mzazi wake ambaye baba mzazi alifurahia na kushukuru baada ya kuingia ukumbini na kukuta marafiki zake wa zamani wameshiriki kwenye hafla hiyo.
“Alinieleza kuwa anawashukuru wageni wote kwa kushiriki hafla hiyo na kwamba imemtia moyo sana kwenye maisha hayo mapya ya kustaafu kwake na aliwaomba waendelee na moyo huo.”alisema Alex Ntonge.