Afisa wa vipodozi ZFDA Mohammed Hassan Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hati ya mashrikiano baina ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA na Shirika la viwango Tanzania TBS huko Ofisi za Wakala wa Dawa na Chakula Mombasa Zanzibar,mashirikiano hayo Yana lengo la kusimamia utekelezaji wa masuala ya udhibiti wa usalama wa Chakula na vipodozi Nchini,ambapo bidhaa itakayosajiliwa upande mmoja wa muungano haitasajiliwa tena upande wa pili.
Mkuu wa usajili na tathimini ya bidhaa za chakula ZFDA Kahadija Ali Sheha akichangia mada wakati wa utolewaji wa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hati ya mashrikiano baina ya Shirika la viwango Tanzania TBS na Wakala wa dawa na chakula ZFDA,hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wakala wa dawa na chakula Mombasa Zanzibar .
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.