********************
Na Victor Masangu,Kibaha
Mbungu wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu kwa kushirikiana na kituo cha Sheria za haki za binadamu wameandaa mafunzo ya siku mbili kwa madiwani wa Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao na kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.
Mafunzo hayo ambayo yamefungwa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo ambayo yamehudhuliwa na madiwani wapatao 54 kutoka halmashauri mbali mbali.
Katika hotuba yake Kunenge aliwata madiwani hao kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kuwatumikia wananchi kwani wao ndio wamesabisha kuwa viongozi hivyo wanapaswa kuwatumikia.
“Madiwani mnatakiwa kuhakikisha mnajituma ili mlete matokeo chanya katika kutatua kero.na changamoto mbali mbali za wananchi na kuweza kusimamia ipasavyo miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika maeneo yenu,,”alisema Kunenge
Aidha Kunenge aliwasisitiza madiwani hao kuweka mipango ya kupigania haki za watoto ,kukemea mimba za utotoni na Mila na desturi ambazo Ni kandamizi ili kupunguza matukio ya aina hiyo ndani ya jamii.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Hawa Mchafu alisema kutokana na matukio ya Mila na desturi zisizo rafiki kwa watoto wa kike,utoro mashuleni na mimba na ndoa za utotoni katika mkoa huo ndicho kilichomsukuma kutafuta ufadhili ili madiwani wapate mafunzo hayo.
Alisema ,amealika madiwani wote 56 wanawake kwa mkoa huo ambao wamejitokeza Ni 54 ambapo Ni sawa na asilimia 96.4.
” Nampongeza Kunenge ,nampongeza na kumshukuru Rais Samia kwa Kuwa wanamaendeleo wa kwanza Mkoani Pwani, Namshukuru Rais kwa kuhakikisha Tisa za bweni zinazotakiwa kujengwa nchini mojawapo itajengwa Mkoani hapa “
” Ujenzi wa shule hizi utakwenda kupunguza mimba za utotoni ,watoto wanapaswa wasome katika Mazingira bora na ya kuwalinda ili kuhakikisha wanasonga kupata taaluma Yao “alisema Mchafu.
Mchafu ,aliwashauri madiwani wanawake kujifunza kuwekeza kabla ya kukoma nafasi zao za Uongozi ilihali wawe na pa kuanzia.
Nae ofisa wa Jinsia (wanawake, watoto na wenye ulemavu kutoka kituo cha haki za binadamu ,Gutruda Dyabene alieleza wametoa mafunzo ya siku mbili ili kujadili changamoto za Uongozi wanazopata madiwani wanawake pamoja na nanma gani wanaweza kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali kama ilivyo kwa wanaume.
Alisema baada ya mafunzo,wataandaa mipango kazi katika Halmashauri zao kufanyia kazi eneo la wanawake, mimba za utotoni,na utoro.
Diwani viti maalum Mjini Kibaha ,Selina Wilson alisema mafunzo hayo yatakwenda kuwasaidia katika majukumu yao .
Aliomba mkuu wa mkoa wa Pwani , kuzungumza na vyombo vya ulinzi na Usalama maana baadhi ya wananchi wanakwama maeneo hayo Mara wanapotaka Sheria itende haki katika kesi za mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia.