Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Bw Abdul Maulid akiwa na Maafisa elimu wa Manispaa za Dar es Salaam pamoja na Wakuu wa Shule za Mkoa wa Dar es Salaam wakiitazama hati ya Uhuru iliyohofadhiwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Afisa Elimu Mkoa wa Dar Es Salaam Bw Abdul Maulid, akifungua kikao kazi cha Maafisa Elimu na Wakuu wa Shule wa Mkoa wa Dar Es Salaam kilichoratibuwa na Makumbusho ya Taifa.
***************************
Na Catherine Ngowi
Maafisa elimu, pamoja na Wakuu wa shule za sekondari na msingi wametakiwa kutumia makumbusho ya Taifa kama nyenzo ya kufundishia ili wanafunzi waweze kujifunza kwa vitendo na kuongeza ufahamu zaidi wa yale wanayo yasoma darasani.
Agizo hilo litolewa Jijini Ilala Dar es Salaam na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Bw Abdul Maulid alipokuwa akifungua semina elekezi iliyolenga kutoa elimu kwa Maafisa Elimu Wilaya pamoja na Wakuu wa shule za sekondari na msingi ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa Makumbusho ya Taifa katika sekta ya elimu na Utamaduni.
Bwana Maulid amesema kuwa wao kama wadau wa elimu wanapaswa kutoa elimu kwa wananchi kupitia wanafunzi hukusu urithi wa Umadanini na Malikale uliopo Makumbusho ya Taifa ili kukamilisha dhana ya kujifunza kwa nadharia na vitendo na hasa kuijua historia ya nchi yao katika harakati za ukombozi hadi sasa ilipo.
“Sisi kama watendaji wa elimu tunaenda kutoa elimu kwa jamii kupitia wanafunzi ambapo ile dhana ya kujifunza kwa nadharia na vitendo itatimia. Nawahamasisha walimu kutumia semina hii kama chachu ya kuongeza uelewa ili tukaitumie kama mabalozi kwa jamii zetu” Bw Maulid.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga ameeleza lengo la semina hiyo kuwa ni kukuza uelewa kwa jamii juu ya urithi wa Taifa unaohifadhiwa hapo hivyo wadau wa elimu nawapaswa kutumia mikusanyo ya kimakumbusho kama zana za kufundishia wanafunzi ili kutimiza lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya urithi wa Taifa na kukuza kizazi cha kizalendo kinachothamini urithi wake na utalii wa ndani.
“Maafisa elimu na walimu ndio wadau wakubwa katika kuhakikisha jamii inapata elimu kupitia wanafunzi hasa wanapotembelea Makumbusho zetu hivyo tunapaswa kukuza uelewa kwa jamii na kuwa na kizazi cha kizalendo na uwajibikaji katika nchi yetu” Dkt Lwoga.
Wakizungumzia mafunzo hayo, Afisa Elimu Taamula Jiji la Ilala na Mwl Angelina Gervas wa Shule ya Sekondari Kambangwa licha ya kuishukuru Makumbusho ya Taifa kwa semina hiyo wamesema sasa watahakikisha ufauli kwenye maneo yao ya kazi unaongezeka kupitia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wao.
“Semina hii imetujenga katika kutunza kumbukumbu za taifa letu na kuwafanya wanafunzi kuwa na hari ya kujisomea na kuijua nchi yao kwa undani pia mahala hapa patakuwa masaada mkubwa kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi”. ameeleza Bi Gervas.
Naye Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Bi Annamary Bagenyi ambeye pia ndio mratibu wa mafunzo hayo, amesema huo ni mwendelezo wa programu ya kuelimisha umma juu ya utajiri mkubwa wa urithi wa Utamaduni na Malikale ulio hifadhiwa katika Matawi ya Makumbusho ya Taifa nchini.