Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.Bahati Geuzye akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.Bahati Geuzye akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es Salaam Afisa habari wa TEA, Bi.Eliafile Solla akiwasilisha mada kwenye semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Huduma za Taasisi (TEA) Bi. Tija Ukondwa akifuatilia Semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es SalaamKaimu Mkurugenzi wa Miradi na Utafutati Rasilimali (TEA) Bi. Anna Makundi akifuatilia Semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es SalaamAfisa Utafutaji Rasilimali na Hamasa Mkuu (TEA) Bw.Hamza Hassan akichangia jambo katika Semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es SalaamMratibu Msaidizi Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (TEA), Bw.Lusungu Kaduma akichangia jambo katika Semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.Bahati Geuzye akiwa pamoja na watuumishi wa TEA wakipata picha ya pamoja na waandishi wa habari katika semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili 1, 2022 Jijini Dar es Salaam
******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), katika mwaka wa fedha 2021/2022 zaidi ya Sh. Bilioni 8.6 ziliidhinishwa kwa ajili ya kugharimia ufadhili wa miradi 160 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini.
Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa madarasa 210 katika shule 70, Maabara 2 za sayansi katika Shule za Sekondari zenye mahitaji maalum, Matundu ya vyoo 2,040 katika shule 80, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na uendelezaji wa miundombinu katika shule za watoto wenye mahitaji maalum.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.Bahati Geuzye wakati akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliofanyika Ofisi za Makao Makuu ya TEA Jijini Dar es Salaam.
Amesema mbali na miradi ya Mfuko wa Elimu wa Taifa, TEA inatekeleza mradi wa miaka 5 (2016/17 – 2020/21) unaotoa ruzuku za utekelezaji wa miradi ya kuendeleza ujuzi kutoka kwenye Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund-SDF).
“Mfuko wa SDF unalenga kuendeleza ujuzi kwa watanzania ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa kwa urahisi na kuchangia uchumi wa Taifa. Mpango umelenga kunufaisha vijana 38,000”. Amesema.
Aidha Bi.Geuzye amesema kupitia mfuko wa Kuendeleza ujuzi kiasi cha Sh. 385,779,984.20 zinatarajiwa kunufaisha vijana 1,018 katika mpango wa Uanagenzi na Utarajari (Internship and Apprenticeship) katika sekta za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Utalii na huduma za ukarimu; Nishati; Ujenzi na Uchukuzi.
Pamoja na hayo amesema Mfuko wa SDF pia unafadhili mafunzo kwa wanufaika 4,000 kutoka Kaya Maskini na Makundi Maalum (Bursary Scheme) hadi ifikapo Juni 2022 na hadi Agosti 2021, jumla ya wanufaika 1,627 walipata mafunzo katika Awamu ya Kwanza ya Mpango huu huku awamu ya Pili ya Mpango wa Ufadhili inatarajiwa kuanza mwezi Aprili 2022, ambapo wanufaika 2,373 wanatarajiwa kupata mafunzo kabla ya Juni 2022.
Hata hivyo ameeleza kuwa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi pia uko katika hatua za mwisho kuanza kutekeleza ufadhili wa mafunzo ya kiubunifu kwa njia ya mtandao (innovative training through e-learning) ambapo umelenga wanufaika 4,305 ifikapo Juni 2022. Kiasi cha Sh. Bilioni 2.3 zitatumika kufadhili mradi huo. Ruzuku ya kiasi cha shilingi 2,321,151,790.00 itawezesha utekelezaji wa mafunzo hayo.