Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kabla ya kufungua Mkutano huo Maalum wa dharura uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga kura kwa ajili ya kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Tanzania Bara Abdulrahman Kinana katika Mkutano Mkuu wa dharura uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.
Viongozi mbalimbali wa Chama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupitisha marekebisho ya Katiba ya Chama ya mwaka 1977 pamoja kumpigia kura kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana leo tarehe 01 Aprili, 2022.