NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Amefungua Jukwaa la wafanyabiashara na Wajasiliamali Wadogo Katika Maonesho yanayo tangulia Kabla ya Ufunguzi wa Mbio za Mwenge hapo April 2 Mwaka huu.
Akifanya Ufunguzi wa Jukwa Hilo la wafanyabiashara katika viwanjwa vya sabasaba mjini Njombe , Wananchi Wameshauriwa Kutumia Furso za Mwenge wa Uhuru Kujikwamua Kiuchumi Kwa Kufanya Biashara Mbalimbali
Wadau mbalimbali akiwemo Meneja Wa Benk ya Nmb tawi la Mkoa wa Njombe Gudluck Shirima Akiwa katika Ufunguzi wa Monesha Hayo amewataka wananchi kutumia huduma za Kibenki kufuata fursa mbalimbali kwani Taasisi hiyo inawafikia ,wafanyabiashara,vyama vya Ushirika na Hata Mtu Moja kupata Huduma Mbalimbali za Kifedha.
Shirima amesema kwatambua fursa za mkoa wa Njombe benki imekuwa ikitoa Mikopo kwa wakulima ya pembejeo,fedha,mashine na mitambo hivyo wakazi wa mkoa huo wanapaswa kuchangamkia huku pia akisema benki hiyo pia inatoa huduma ya bima ya mazao
Aidha Wito Umetolewa Kwa Wajasiliamali Kukimblia fursa zinazo tolewa wakiwemo wakulima ambao wamekuwa katika changamoto kubwa ya Kupata Pembejeo za Kilimo.