Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mbunge wa Jimbo, la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Ujenzi wa Kituo Cha Afya Kongowe ,kitakachogharimu Tsh Mil .400 hadi kukamilika kwake.
Akiwa katika eneo la tukio, Koka amezisisitiza kamati za usimamizi wa Ujenzi huo kuwa wazalendo na kuheshimu pesa ya serikali huku akihimiza miradi kukamilishwa kwa wakati lengwa.
Hata hivyo amewataka wajumbe wa kamati hizo na Viongozi kusimamia Ujenzi sambamba na kuzingatia thamani ya pesa.
Koka alieleza, kituo hicho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Kibaha, ambapo kinatarajiwa kukamilika Julai Mwaka huu na kuwanufaisha wakazi wa kata ya Kongowe na maeneo jirani.
Pamoja na hilo, alialikwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kata ya Kongowe kuwa Mgeni rasmi na amewapongeza Viongozi wote wanaomaliza muda wao, na kuwahamasisha wanachama wenye nia wagombee kwa uadilifu Ili kuendelea kukijenga na kukiimarisha chama .
Vilevile amegawa vyeti kwa wanachama na Viongozi mbalimbali wa kata hiyo waliofanya kazi za chama vizuri, akiwemo diwani viti maalum Kibaha, Lidya Mgaya, vyeti ambavyo vilivyoandaliwa na Kamati ya siasa ya kata hiyo ,:;Pia Koka amekabidhi viti 25 vya plastiki vyenye thamani ya Tsh 450,000/- kwenye mradi wa Vijana wa kata hiyo.