Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akifungua Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi.Doreen Sinare akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw.Elia Mjatta akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Mkuu wa idara ya Uhusiano Multichoice Tanzania Bw.Johnson Mshana akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Bi.Angella Mang’enya akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatilia Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa COSOTA katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Mwakilishi kutoka Tume ya Ushindani (FCC) Bi.Khadija Ngassosywi akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Mwanasheria COSOTA Bw. Lupakisyo Mwambinga akiwasilisha mada katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.Mwanasheria COSOTA Bw.Zephania Lyamuya akiwasilisha mada katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu wizara ya utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas amewataka Watanzania kutumia ubunifu wao vizuri na kuulinda kisheria ili waweze kunufaika kiuchumi.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo ya siku moja ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari huku akisema dhana nzima ya hakimiliki ni kulinda ubunifu wa wahusika katika hakimiliki na hakishiriki.
“Kwenye nchi zilizoendelea Hakimiliki imekuwa sehemu kubwa sana ya kipato na sehemu ya kuboresha maisha ya watu na kuongeza chachu ya watu kuendelea kubuni vitu mbalimbali ambavyo pia huingia kwenye ushindani”. Amesema Dkt.Abbasi.
Dkt.Abbasi amesema Serikali kwa kioindi cha mwaka mmoja wametimiza wajibu wake kwa kuendelea kuboresha mazingira mbalimbali ya kusaidia watanzania kunufaika.
Aidha Dkt.Abbasi amesema Serikali imeongeza fedha za usimamizi na uendeshaji wa masuala ya taasisi ya COSOTA ili nao wakusanye fedha na wanaopaswa kupata fedha zao wapatiwe.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi.Doreen Sinare amesema COSOTA imeweza kulipa Mirabaha kwa Wasanii 1,123 ambapo kwa mara ya kwanza na hii ni idadi kubwa, tangu kuanzishwa kwa COSOTA.
“Hakuna kipindi Wasanii wengi kiasi hichi wamelipwa mirabaha yao tena kwa kuzingatia utaratibu wa Kimataifa wa matumizi ya kazi zao katika maeneo ya biashara”. Amesema Bi.Doreen.
Amesema jumla ya kazi 5,924 ambazo ni nyimbo za wasanii zilizotumika katika vituo vya redio saba zilitumika kama sampuli kufanya mgao wa mirabaha.
Pamoja na hayo Bi.Doreen amesema COSOTA imefanikiwa kupata fedha ya miradi ya maendeleo ya taasisi ambazo zimesaidia kuboresha huduma za taasisi kwa kutengenezwa kwa mfumo wa kidijiti wa Utoaji wa Leseni za Matumizi ya kazi za Ubunifu, Usajili wa kazi za Ubunifu na kujiunga uanachama kwa wadau na kusajili kazi za ubunifu kwa njia ya mtandao popote walipo bila kuhitajika kufika ofisi za COSOTA.