Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Salma Ali Hassan akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusu taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii hasa Whatsaap kuhusu masikitiko ya kupewa dhamana mshtakiwa Khator Said Hamad ambae anakabiliwa na tuhuma ya mauaji ya mke wake Zulfat Shekhan ,huko Ofisini kwake Miembeni Mjini Unguja. Mkurugenzi Salma amesema kwa mujibu wa kifungu cha 152(1)cha sheria ya makosa ya jinai mabano (nam 7/2018)kinataka kesi ianze kusikilizwa ndani ya miezi sita baada ya mshtakiwa kukamatwa, na iwapo kesi haijaanza kusikilizwa ndani ya miezi sita mshtakiwa ana haki ya dhamana na hilo ndilo lililofanyika.
PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR.