Shodadi Katuya (32) ni mzaliwa wa Mtama ni fundi ujenzi aliyehitimu aliyehitimu Ndanda anamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kupeleka mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kwa kuwa yeye ni kati ya vijana walionufaika na mradi huo kwa kushiriki katika ujenzi wake.
“Kuna vijana wengi wameacha kuzulura mtaani wako hapa wametengeneza ajira zao kama ulivyoona huko nje na licha ya hivyo tu, imewakomboa watu katika mambo mengi kipindi hichi cha kilimo watu wameacha kutumia jembe la mkono amechukua hela yake ya kibalua hapa ameenda kuweka kule kwenye matreka amelima heka tatu, heka nne heka tano na anaendelea na kazi hapa,”alisema Shodadi.
Hakuishia hapo tu, Shodadi amesema kwamba tenda aliyoipata ya ujenzi wa kituo hicho imemsaidia kuweza kununua bodaboda yake na kuendeleza maisha yake.
“Mimi mwenyewe sasa hivi namiliki bodaboda yangu binafsi kupitia tu miradi hii hapa na tunamshukuru sana mama Samia kwa sababu sekta aliyoishika hii ni sekta ya afya ambayo inamgusa kila mmoja wetu, kiasi kwamba kutuletea Mtama tunahisi kama ametupendelea …tuna kila sababu ya kumshukuru na tunamshukuru sana tu,” alisema Shodadi.
Tenda ya ujenzi wa kituo hiko cha afya aliipata kutoka kwenye Halmashauri baada ya tangazo kutoka nayeye kupeleka barua ingawa hakuwa na uhakika kama angepata kazi hiyo kwani walikuwa waombaji wengi.