Kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo Bernard Biswalo akifanya malipo kwa moja ya mteja aliyekuwa anadaiwa ankara ya deni la maji la miezi ya nyumba
Na Lucas Raphael,Tabora
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inadai zaidi ya sh mil 600 ambazo ni malimbikizo ya madeni ya wateja wake ya muda mrefu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani Tabora Kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo Bernard Biswalo kwenye siku ya maji dunia kufuatia za mwenendo wa malipo ya ankara za maji yalifayika kwa kutembelea wateja mbalimbali wanaodaiwa bili za maji mitaani na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya maji nyumbani .
Alisema kwamba baadhi ya wadaiwa sugu wameshakatiwa huduma hiyo huku deni la wateja wanaoendelea kutumia huduma ya maji kwa sasa limefikia kiasi cha shilingi milioni 430.
Hata hivyo akiongelea upande wa Taasisi za umma na serikalai alisem kwamba wanadaiwa hadi sasa kiasi cha shilingi bilionil 1.7.
Alisema mamlaka inadai fedha nyingi sana kutoka sehemu kwa ajili ya huduma waliyoitoa ya maji kwenye nyumba Taasisi za serikali na za umma .
Biswalo alisema kwamba kwa sasa Tuwasa itakuwa na utaratibu wa kupita nyumba kwa nyumba mtaa kwa mtaa kudai madeni yake kila mara baada ya Ankara za maji kutoka.
“Kinachoonekana hapa ni wateja wetu kushindwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya maji ili kulipa bili zao kwa wakati jambo ambalo linakwamisha shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo”alisema Biswalo
Alisema licha ya kudai pia wataendelea kutoa elimu sahihi ya matumizi bora ya maji safi na maji taka ambapo huduma hiyo imekuwa itolewa na mamlaka hiyo.
Aidha Kaimu Mkurungezi huyo alitoa wito kwa wateja wote wanaodaiwa malimbikizo ya madeni ya ankra zao kulipa kwa wakati ili kuepusha usumbufu ikiwemo kukatiwa huduma hiyo au kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mamlaka ya Tuwasa waliitimisha kilele cha wiki ya maji kwa kutembelea wateja wanaopata huduma ya maji na kutoa elimu ya matumizi bora ya maji Nyumbani wiki ya maji ilikuwa na Kauli mbiu Isemayo “Maji chini ya ardhi -Hazina Isiyoonekana kwa Maendelep Endelevu “