Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza na watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza na wajumbe wa wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet Hasunga na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Yahaya Mgawe
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao na watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Mheshimiwa Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya Utafiti wa Samaki iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo-Uvuvi kuwa asimamie vyema mradi Maabara ya Utafiti ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati.
Agizo hilo limetolewa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Joseph Hasunga wakati walipotembelea kukagua mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Utafiti ya TAFIRI iliyopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Hasunga ameisihi wizara hiyo kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa Wakati na kufikia malengo ya Serikali ya kufikia Uchumi wa bluu Kupitia Sekta ya Uvuvi.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na UVuvi Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, amesema kuwa Mradi huo wa Ujenzi wa Maabara ya Utafiti mara baada kamilika Utaleta tija katika sekta ya Uvuvi ikiwemo kusaidia kutambua idadi ya Samaki wanapopatikana na kushughulikia maswala ya uvuvi.
Amesema kuwa wamepokea maelekezo ya kamati ya Bunge na kuhakikisha watafanyia kazi ili waweze kufikia malengo yaliyowekwa.