Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi wa Unganda nchini Mhe. Richard Kabonero ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Unganda nchini Mhe. Richard Kabonero ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi Balozi wa Unganda nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi Mhe. Richard Kabonero katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akishiriki katika Mkutano wa Nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ulifanyika kwa njia ya mtandao. Mkutano huo umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angloa na Mwenyekiti wa ICGLR Balozi Tete Antonio
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akionge na Mabalozi (wastaafu) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
…………………………………………………..
Na Waandishi Wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amemuaga Balozi wa Unganda nchini Mhe. Richard Kabonero ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mulamula amempongeza Balozi Kabonero kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuendeleza na kudumisha uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Uganda.
Waziri Mulamula ametaja baadhi ya mafanikio ambayo yamepatika katika kipindi cha uwakilishi wake hapa nchini, kuwa ni pamoja na kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Choleani, Tanzania lenye urefu wa Kilomita 1443 na kukua kwa urari wa biashara kati ya Tanzania na Uganda.
“Serikali kwa ujumla tunashukuru zaidi kwa ushirikiano uliotuonesha wakati wote ulipokuwa hapa kama Balozi na tunakuahidi kuudumisha na kuuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi ya nchi zetu mbili (Tanzania na Uganda),” amesema Balozi Mulamula.
Kwa upande wake Balozi Kabonero ameishukuru Serikali kwa kumpatia ushirikiano wakati wote alipokuwa akitekeleza majukumu yake hapa nchini.
“Naomba kuishukuru sana Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mlionipatia wakati wote nilipokuwa hapa kama balozi, kwa kweli nilifarijika sana kuwa nanyi……..naahidi kuwa balozi mwema wa Tanzania asante sana,” amesema Balozi Kabonero.
Tanzania na Uganda zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, nishati, elimu, pamoja na usafirishaji.
Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika Mkutano wa Nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ulifanyika kwa njia ya mtandao na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angloa na Mwenyekiti wa ICGLR Balozi Tete Antonio.
Pia Waziri Mulamula ameshiriki kufunga Mkutano wa Mabalozi (Wastaafu) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.