Mollahan Kabonde wakili wa kujitegemea akizungumzia maendeleo mbalimbali yaliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu
**********************
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Wakili wakujitegemea kutoka ofisi ya Kabonde & Magoiga Law Firm iliyoko Jijini Mwanza, Mollahan Kabonde amezungumzia mafanikio aliyoyafanya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu katika kipindi chake cha mwaka mmoja katika uongozi wake.
Akizungumza leo hii Machi 24, 2022 ofisini kwake Kabonde amesema kuwa amefurahishwa sana kwa namna ambavyo anaendeleza miradi mbalimbali iliyoachwa na mtangulizi wake hayati John Magufuli.
Amesema kuwa Kwa Mkoa wa Mwanza Mh. Samia Suluhu ameendelea kutekeleza miradi mingi ikiwemo, Ujenzi wa Meli mpya, ukarabati wa Meli za MV. Umoja, MV. Clarias pamoja na ujenzi wa Meli mpya inayo endelea kujengwa katika karakana ya ujenzi wa Meli eneo la Mwanza Kusini.
Kabonde ameeleza kuwa miradi hiyo imekuwa chachu ya maendeleo kwa Wananchi kwani imetoa ajira kwa vijana.
“Binafsi nazidi kumpongeza sana Rais wangu kwani kwa huu mwaka mmoja wa uongozi wake kazi aliyoifanya inaoneka, nazidi kumuombea ili awe na afya njema na azidi kulitumikia Taifa kwa amani na utulivu”, amesema Kabonde.
Ameeleza namna ambavyo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu alivyo fungua vituo mbalimbali vya shule za awali ambazo zimepunguza changamoto ya watoto kubanana kwenye darasa moja.
Mwisho Kabonde ametoa ushauri kwa wanawake kufuata nyao za Rais Samia ili wawe na uthubutu wa kufanya mambo katika nyanja mbalimbali za uongozi hususani kwa wale ambao wanateuliwa ili waweze kuendana na kasi yake katika kutekeleza maendeleo.