Kutoka Kushoto: Balozi Maimuna Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu, Geneva, Mh. George Simbachawene Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Hoyce Temu Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva na Nkasori Sarakikya Mkurugenzi Wizara ya Katiba na Sheria
********************
Tanzania yahudhuria Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu, ambapo Tanzania (JMT) imefanyiwa tathmini ya Haki za Binadamu.
Waziri wa Katika na Sheria Mhe. George Simbachawene ameongoza Ujumbe wa Tanzania ambapo ameeleza hatua mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye masuala mbalimbali ya Haki za Binadamu nchini Tanzania ikiwemo Elim, Afya, Haki za Watoto, Wanawake, wenye ulemavu, Haki za Kisiasa na mengine mengi.
Tathmini ya Tanzania imekubaliwa na Baraza hilo, nchi 23 zilizoizungumzia Tanzania kwa hatua nzuri zilizofanyika katika kuhakikisha Haki za Binadamu zinazingatiwa. Pia wamekumbusha Tanzania kuendelea kutatua changamoto zilizobaki.