Meneja wa mradi wa Uviko 19 Mhandisi Thomas Msenyele akizungumza na vyombo vya habari eneo la Tukio.
………………………………
Na Lucas Raphael,Tabora
Serikali kupitia Mpango wa ustawi wa Maendeleo wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19 imeiwezesha mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tabora TUWASA kiasi cha shilingi million 547 kwa ajili mradi wa kusambaza maji kwenye maeneo yaliopo pembezoni mwa manispaa hiyo .
Kauli hiyo ilitolewa jana katika siku ya kilele cha wiki ya maji Dunia manispaa ya Tabora na Meneja wa mradi wa Uviko 19 Mhandisi Thomas Msenyele mara baada ya kutembelea usambazaji wa bomba na unganishaji wa maji nyumbani katika kidogoji wa Kidatu B kata ya mtendeni wilaya ya Tabora mkoani Tabora.
Alisema kwamba Mradi huo wa maji unatarajia kuwafikia wateja 1000 na wanufaika ni zaidi ya 12,000 katika maeneo ya Kidatu A, Rada ,Kidatu B ,Ikindwa, Malolo Utusini,Ulamba,Mawiti ,Misha Mfangajini, Kilumbo ,Mtakuja na Changombe ambao wanaunganishiwa maji kwa kiasi cha ashilingi 100,000 tu.
Alisema kwamba mradi huo ulionza machi 22 mwaka huu katika eneo la Kidatu B utararijia kusambaza mabomba umbali wa kilometa 42.055 za kulaza bomba na kuwafikia walengwa waliokusudiwa kupata huduma maji safi na salama kupitia mradi wa uviko 19 manipaa ya Tabora.
Alisema kwamba hadi sasa Fedha zilizopokelewa ni kiasi cha shilingi milioni 367 kwa awamu ya kwanza ambapo hadi mradi utakapo kukamilika utagharimu jumla ya shilingi million 547.
Alisema kwamba kutokana na kazi inayoendelea wanatarajia kukamilisha mradi huo ifikapo Juni 30 mwaka huu na tayari umetelekezwa kwa asilimia 25 tu.
Nao baadhi ya wanufaika wa mradi huyo wa maji ambao ni Leokadia Alois na Rashid Omari walishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha na kuwawesha kuunganishwa maji katika nyumba zao kwenye kilele cha siku ya maji dunia .
“jambo hili ni njema sana kwani walikuwa wanatumia maji ya kisima kwa muda mrefu lakini kwa sasa wanatumia maji ya kutoka kwenye bomba tena kwa ghrama ya shilingi 100 ,000/tu”
Hata hivyo waliwaomba wananchi wenzao wanaishi maeneo mbalimbali unakopita mradi huo kuunganisha maji ili kupunguza muda wa kufanya shughuli zingine za Kiuchumi na kujenga taifa .
Kauli mbiu ya wiki ya maji mwaka huu ni “Maji chini ya Ardhi –hazina Isiyoonekana kwa Maendeleo Endelevu”