Meneja wa mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya ziwa, Dkt. Iragi Ngerageza akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kampeni ya uchangiaji damu.
Ally Hussein mkazi wa Buhongwa akichangia damu katika kituo cha benki ya damu salama kanda ya ziwa
Mazao ya damu salama yaliyohfadhiwa kwenye maabala ya benki ya damu salama kanda ya ziwa.
**********************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Serikali imeshauriwa kuongeza nguvu katika kuelimisha jamii ili wafahamu umuhimu wa kuchangia damu hali itakayo saidia kupunguza uhaba wadamu unaoikabili benki ya damu salama kanda ya ziwa.
Ushauri huo umetolewa leo mara baada ya mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kampeni ya uchangiaji damu salama yenye kauli mbiu, “Damu ni dhahabu nyekundu yenye utajiri wa uhai”.
Wakizungumza na Fullshangwe kwa nyakati tofauti wachangiaji damu Minza Saidi na Ally Husen, wamesema elimu juu ya umuhimu wa kuchangia damu salama inatakiwa zaidi kutokana na uhaba uliopo.
Wamesema elimu itolewe makundi kwa makundi ili kupunguza ukubwa wa tatizo kwani wakati huu damu inahitajika kwa wingi hasa kwa akina mama wanaojifunguwa na majeruhi.
Kwa upande wake meneja wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya ziwa, Dkt Iragi Ngerageza amesema lengo la Taifa ni kukusanya lita 100,035 kwa kila kanda kwa mwaka, lakini hadi sasa benki hiyo imekukusanya lita elfu 60,000kwa kipindi cha miezi minane.
Amesema Jamii kupitia makundi yao wakiwemo wafanyabiashara wa sokoni,vikundi mbalimbali vya vikoba na wanandugu wakiunda vikundi vya wachangiaji damu salama itasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa damu salama sanjari na kuokoa watu wenye uhitaji.
Dkt Ngerageza ametoa sababu ya upungufu huo kuwa unatokana na kundi kubwa la wachangia damu ambao ni wanafunzi wa sekondari kwa hivi sasa wamepoteza sifa ya kuchangia damu kwa sababu wanakuwa chini ya umri wa miaka 18.
“Tunalazimika kutegemea kundi la wanafunzi wa kidato cha tano na sita ambao tayari wapo katika umri wa kuchangia lakini wakati mwingine wanakosekana kwasababu ya kuwa likizo ambayo ni Juni na Desemba”, amesema Ngerageza.