Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Ridhiwani Kikwete
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, (Mb) wa Chalinze amesema wananchi wa Chalinze wameweka historia ya kupata maji ya uhakika baada ya kuteseka miaka mingi kwa kukosa maji safi na salama.
Amewashukuru Rais John Magufuli na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa wa Maendeleo walioufanya na hasa mchango wao kwenye mradi wa Maji wa Ruvu-Mboga.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokez katika viwanja vya Polisi Chalinze, Mh. Kikwete alisema, “…anamshukuru sana Hayati, Rais John Pombe Magufuli kwa kutupatia Shilingi bilioni 8 kwa ajili ya kuanzisha mradi huu wa maji. Pia Tunakushukuru wewe
Mhe. Rais kwani ndani ya kipindi cha mwaka mmoja umeidhinisha Shilingi bilioni 11 na kufanya mradi huu kuwa
na gharama ya Shilingi bilioni 19 ili mradi huu ukamilike mapema iwezekanavyo.”
Wananchi mbalimbali waohojiwa na mwanahabari wameshukuru sana hatua stahiki zilizochukiliwa na Mh. Rais hasa kutatua shida kubwa ya maji.