Ndege kubwa mali ya shirika la ndege la Eastern Airlines la China iliyokuwa imebeba watu 132 kwenye jimbo la Guangxi, maafisa wa China wamethibitisha.
Kwa mujibu wa Shirika la Anga la China (CAA), Ndege hiyo ilikuwa na abiria 123 na watumishi 9.
Bado taarifa rasmi za chanzo cha ajali hiyo na kiwango cha athari hakijafahamika.
Shirika la habari la China limedai kuwa ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ilipata ajali kwenye mji wenye milima wa Wuzhou, huku mlipuko wa moto ukishuhudiwa kwenye mapori.
Tayari vikosi vya uokoaji vimeshatumwa kwenda kutoa msaada kwenye eneo hilo.
Ndege hiyo yenye usajili wa MU5735 iliondoka kwenye mji wa Kunming saa 7:11 mchana kwa saa za China na ilitarajiwa kuwasili kwenye mji wa Guangzhou saa 9:05.
CHANZO:AZAMTV