Katibu tawala wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara Daniel Zenda kulia,akizungumza wakati wa utiliaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira(Ruwasa)mkoa wa Mtwara ambayo inakwenda kutekelezwa katika wilaya hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni 4.5,kushoto Meneja wa Ruwasa mkoa wa Mtwara Mhandisi Primy Damas.
Menaja wa wakala wa Usambazaji maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)mkoa wa Mtwara Mhandisi Primy Damas kulia,akimkabidhi mkataba wa ujenzi wa miradi miwili ya maji Mkurugenzi wa Kampuni ya Nandra Enginering Contruction Co Ltd Malkiti Nandra wa pili kushoto,miradi inayotarajia kutekelezwa katika Halmashauri mbili za Newala vijiji na Halmashauri ya Mji Newala,anayeshuhudia katikati Katibu Tawala wa wilaya hiyo Daniel Zenda.
Katibu Tawala wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara Daniel Zenda katikati,Meneja wa Ruwasa mkoa wa Mtwara Mhandisi Primy Damas wa pili kulia na Mwakilishi wa kampuni ya Nandra Enginering Contruction Co Ltd Malkiti Nandra wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalam wa wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) baada ya Ruwasa na kampuni ya Nadra kusaini mikataba miwili ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni 4.5 miradi inayotarajia kutekelezwa wilayani humo.
…………………………
Na Muhidin Amri,
Newala
WAKALA wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa) mkoa wa Mtwara,umesaini mikataba miwili ya ujenzi wa miradi mipya ya maji yenye thamani ya Sh.bilioni 4.5 ili kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo katika wilaya ya Newala.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo Katibu Tawala wa wilaya Daniel Zenda, amemtaka mkandarasi kujenga miradi hiyo kwa viwango na ubora ili iweze kuleta tija ya kumtua mama ndoo kichwani na kumaliza kero ya upatikanaji wa huduma ya maji kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Aidha,amemkumbusha suala la uadilifu,kutanguliza uzalendo na kuepuka ubabaishaji katika kutekeleza miradi hiyo na kuonya kuwa ,Serikali haitosita kumchukulia hatua kali iwapo atashindwa kutekeleza miradi kwa ubora unaotakiwa.
Amemtaka kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza ujenzi wa miradi hiyo,ili wananchi walioteseka kwa muda mrefu waweze kupata huduma karibu na makazi yao na kuwapunguzia muda wa kutembea na kwenda mbali kutafuta maji.
“miradi hii haihitaji ubabaishaji,tunataka miezi sita ya mkataba itumike kuleta maji katika wilaya yetu ya Newala, katika ujenzi wa miradi hiyo nakumba sana sana zingatia ubora ili iendane na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na Serikali”alisema Zenda.
Alisema,katika wilaya ya Newala kuna changamoto kubwa ya maji safi na salama kutokana na uchakavu wa miundombinu iliyojengwa kwa muda mrefu hali iliyosababisha upatikanaji wa huduma ya maji kuwa mdogo.
Kwa mujibu wa Zenda,kujengwa kwa miradi mipya itasaidia sana kupunguza kama sio kumaliza changamoto ya maji ambayo imewatesa wananchi wa wilaya hiyo kwa muda mrefu.
Pia,amemuomba mkandarasi kufanya kazi kwa mujibu wa mkataba na kupeleka mpango kazi wake Ofisi ya Mkuu wa wilaya ili serikali iweze kufuatilia na kuchukua hatua pindi kazi itakapotekelezwa kinyume na makubaliano yaliyopo katika mkataba.
Alisema,serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, itahakikisha inasimamia kwa karibu ujenzi wa miradi hiyo ambapo amemtaka mkandarasi kuwashirika viongozi wa ili atakapokwama waweze kumsaidia.
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa mkoa wa Mtwara Mhandisi Primy Damas alisema, muda wa utekeleza wa miradi yote miwili ni miezi sita na inatekelezwa katika Halmashauri ya mji wa Newala na mwingine utatekelezwa katika Halmashauri ya wilaya Newala.
Kwa mujibu wa Damas mradi unaotekelezwa Newala mjini una gharama ya Sh.bilioni 2,443,332,684.10 na wa Newala vijijini una thamani ya Sh. bilioni 2,101,675.296.
Alisema, miradi hiyo itakapokamilika itasaidia kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa wilaya ya Newala na kuishukuru Serikali kupitia wizara ya maji chini ya Waziri Jumaa Aweso kutoa fedha hizo za kutekeleza miradi hiyo.
Kwa upande wake, Mkandarasi anayepewa kazi ya kujenga miradi hiyo kampuni ya Nandra Enginerering Construction Co Ltd Malkiti Nandra amehaidi kufanya kazi kwa viwango na na kumaliza kwa muda uliopangwa.