Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya dkt.Salum Slim akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umoja wa madaktari waliojitolea kuwahudumia wananchi wa mkoa Kusini Unguja katika zoezi maalum la kuwapatia huduma za matibabu bila malipo ndani ya kituo cha Afya kilichopo Kidimni wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ,zoezi hilo liliratibiwa na Baraza la Mji Kati.
Mkurugenzi Baraza la Mji Kati Salum Mohammed Aboubakar akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la upatikanaji wa huduma za Afya bila malipo katika kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ,wakati zoezi hilo likiendelea .
Mwandishi wa Habari gazeti la Zanzibar leo ambae pia ni mkaazi wa kibele Mkoa wa Kusini Unguja Madina Issa akipatiwa huduma ya Afya ya macho katika Kituo cha Afya Kidimni wakati wa zoezi la utoaji wa huduma bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja liloratibiwa na Baraza la Mji Kati.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)dkt.Ibrahim kabole akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi wa Shehia mbalimbali za Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wakisubiri kupatiwa huduma za Afya kutoka kwa madaktari mbalimbali wa Umoja wa Madaktari , wakati wa zoezi la utowaji wa huduma za Afya bure katika kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –ZANZIBAR.