Mwandishi wa vitabu kama “Mimi na Rais” pamoja na Chochoro za Madaraka Bw. Lello Mmasy akikabidhiwa kitabu cha VIJANA WA KIKRISTO na mtunzi wa kitabu hicho Bw.Mwijarubi Mwijarubi mara baada ya kukizindua leo tarehe 18/03/2022 Jijini Dar es Salaam Mwandishi wa vitabu kama “Mimi na Rais” pamoja na Chochoro za Madaraka Bw. Lello Mmasy akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha VIJANA WA KIKRISTO Leo Jijini Dar es Salaam.Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Richard Hananja akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha VIJANA WA KIKRISTO Leo Jijini Dar es Salaam.Mtunzi wa kitabu cha VIJANA WA KIKRISTO Bw.Mwijarubi Mwijarubi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu chake leo tarehe 18/03/2022 Jijini Dar es Salaam
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Vijana nchini wameaswa kupendelea kusoma vitabu ili kutokuwa watumwa wa kifikra na kuweza kusimamia ndoto zao za kimaisha na kuondokana na umasikini.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu chake Kiitwacho VIJANA WA KIKRISTO na changamoto na utatuzi wake, Bw. Mwijarubi Mwijarubi amesema kuwa vijana wengi hawachukui muda wao kusoma na kujifunza mambo mengi ya kukabiliana na maisha na changamoto zake hivyo kupitia kitabu hicho kitaweza kuwasaidia kupambana nazo na kuzitatua.
“Kitabu hiki kimegawanyika katika changamoto za vijana katika makundi makuu manne ambayo yamefafanuliwa kwa ufupi katika Afya,Uchumi, Utandawazi na Mahusiano”. Amesema Bw.Mwijarubi.
Kwa upande wake mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Richard Hananja amewataka vijana kutumia kitabu hicho kama sehemu ya kutatua na kupambana na changamoto za maisha.
Naye Mgeni wa heshima katika uzinduzi wa kitabu hicho Lello Mmasy ambaye ni Mwandishi wa vitabu kama “Mimi na Rais” pamoja na Chochoro za Madaraka amesema kwamba kila kijana atakayesoma kitabu hicho kitambadilishia matanzamo wake katika maisha yake.