*******************
NJOMBE
Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa (USEMI) imepongeza kazi kubwa inayofanywa na halmashauri ya wilaya ya Njombe katika utekelezaji wa miradi ikiwemo ya afya wilayani humo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Abdallah Chaurembo ametoa pongezi hizo kwa niaba ya kamati mara baada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ukiwemo ujenzi wa kituo cha afya Mtwango unaojengwa kwa mapato ya fedha za ndani.
“Nimpongeze mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ameonyesha kwa vitendo kumsaidia Rais wetu,Kamati imeona kiasi cha fedha inayotumika na ujenzi unaoendelea wa kituo cha afya Mtwango,mkurugenzi amefanya wajibu wake”amesema Abdallah Chaurembo
Aidha kamati imeelekeza kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha halamshauri zao zimetekeleza maelekezo ya kamati hiyo.
“Natoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini,wiki mbili zajazo wanakuja kwenye bajeti tunataka kuona maelekezo tuliyotoa kamati ya kujenga kituo cha afya,tupate taarifa ya vituo vya afya vinavyofanana na hiki cha Mtwango”Abdallah Chaurembo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi,Sharifa Nabarang’anya amesema malengo ya halmashauri katika ujenzi wa kituo hicho kinachoghalimu zaidi ya milioni 900 ni kuhakikisha kinakamilika katika bajeti ya msimu ujao ili kweze kuanza kutoa huduma.
“Robo ijayo tutamalizia kiasi cha fedha iliyobakia ili kukamilisha ujenzi wa kituo kizima cha afya”alisema Nabarang’anya
Kamati ya bunge,utawala na serikali za mitaa (USEMI) imetembelea na kukagua miradi mitatu ya ujenzi wa kituo cha afya Mtwango,kituo cha cha afya cha Ilengititu kilichojengwa kwa msaada wa fedha za TASAF pamoja na mradi wa kusaga kokoto wa kikundi cha vijana uliopo Mtwango na kuridhishwa na miradi hiyo.