********************
Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ,John Palingo ameitaka mamlaka ya maji safi na na usafi wa mazingira kanda ya Sikonge Kusitisha huduma ya maji kwa wateja wenye madeni makubwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wateja sugu ili kuhakikisha wanalipa madeni hao.
Kauli hiyo aliitoa jana kwenye mkutano na wadau wa maji mjini Sikonge wenye lengo la kutoa elimu juu ya matumizi bora ya rasilimali maji kwa wananchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha maendeleo ya wananchi wilayani humo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mamlaka imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuwapatia huduma ya maji wateja wake lakini mara baada ya kupata huduma ya maji wamekuwa wagumu kulipa kwa wakati hivyo ifikie kila mtu anatimiza wajibu wa kulipa bili ya maji .
Alisema kwamba hadi sasa mamlaka hiyo inazidai jumla ya deni kwa Taasisi za serikali na watu binafsi hadi kufikia desemba 2021 kiasi cha silingi milioni 23,990,783
“Katika wiki ya hii ya maji Taasisi za umma, ikiwemo ofisi yake na wadaiwa wengine katika wilaya ya Sikonge kuakikisha wanalipa madeni yao ili huduma ya maji iendelee kutolewa mamlaka hiyo “alisema mkuu wa wilaya ya Sikonge Jon Palingo.
Alisema kwa madeni hayo napaswa kulipwa haraka ili mamlaka hiyo iweze kujiendesha kwani kwa sasa inajiendesha kwa hasara.
Alisema kwamba mamlaka hiyo inapata Mapato ya wastani wa Tsh. 11,000,000 kwa mwezi ukilinganisha na matumizi ya Tsh. 17,000,000 kwa mwezi .
Palingo alisema kwamba madini hayo ni wilaya ya Sikonge pekee lakini madeni hayo ni mengi ukilingani huduma zinazotolewa na mamlaka katika makao makuu ya manispaa ya Tabora ,Urambo na wilaya ya Uyui mkoani hapa .
Nae Kaimu Mkurungezi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Tabora Tuwasa, Bernard Biswalo alimweleza mkuu huyo wa wilaya ya Sikonge kwamba kwamba mamlaka hiyo inakabiliwa madeni mbalimbali ambapo fedha zote zipo kwa wateja ambao wameshindwa kulipa madeni yao kwa wakati.
Alisema kwamba ili mamlaka hiyo iweze kujiendesha ni lazima madeni hayo yalipwe haraka ili mamlaka hiyo iweze kujiendesha kwa ufanisi .
Akizungumzia mafanikio ya mamlaka hiyo Biswalo alisema kwamba lengo ni Kuboresha upatikanaji wa maji kwa wastani wa saa 6 kutoka saa 3 kwa siku na kuongeza wateja kutoka 472 hadi 657 mwaka .
Alisema kwamba jitiada zingine ni kuongeza Mauzo ya maji kutoka lita 40,469,000 hadi 58,790,000 kwa mwaka pamoja Kupandisha makusanyo kutoka shilingi miloni 67,649,741 hadi 157,180,564 kwa mwaka.
Biswalo aliendelea kusema kwamba wamekusudia kuondoa magugu bwawani kwa wastani wa 20% na Kuboresha mazingira ya kituo cha uzalishaji maji kwenye cha Bwawa la Utyatya .