Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Sara Msafiri ameahidi kuendelea kuvalia njuga changamoto za wawekezaji ,na kuangalia vikwazo vya soko Lao la ndani ili kunufaika na uwekezaji nchini .
Ameeleza moja ya changamoto Ni Pamoja na viwanda vya gypsum kuzalisha kwa wingi bila tija kutokana na wawekezaji wa gypsum nje ya nchi kulipa kodi ndogo na kusababisha wawekezaji wa ndani kukosa soko kubwa.
Akitembelea kiwanda cha Jafra Investment and Supplies Company Limited, BNBM Tanzania,Pwani Steel na Hong Yu Steel Company Limited ambavyo vinazalisha vifaa mbalimbali vya ujenzi katika ziara yake maalum Zegereni, Kibaha alisema ,Lengo ni kutambua vikwazo vyao na baada ya ziara atafikisha kwenye Mamlaka husika kufanyiwa kazi.
Mkuu huyo wa wilaya , alisema ziara hiyo imelenga pia kujiridhisha kama kama viwanda vinafanya kazi zao kwa malengo waliyojiwekea pasi na changamoto yoyote itakayokwamisha uzalishaji
na malengo kufikiwa.
“Nimetembelea viwanda vilivyopo Kibaha kujionea kama viwanda hivyo vinafanya kazi zao kwa malengo waliyojiwekea? Na kama kuna changamoto ni zipi ili tuzitatue?, haya yote ni katika kuhakikisha kwamba yale malengo ya kuanzishwa kwa viwanda yaweze kutimia” alisema Sara .
“Tunaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu maeneo ya viwanda. Hapa Zegereni, reli ya kati na ya kisasa itafika, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) nao wana mpango wa kuivuta gesi hadi kufika eneo la Zegereni, pia tunatarajia kuwa na njia maalum ya umeme,maji na gesi eneo la viwanda”
Wakiongea kwa nyakati tofauti, afisa mahusiano wa BNBM Prosper Ernesty pamoja na Mepsedeck Piason ambae ni afisa Raslimali watu na Utawala kiwanda cha Jafra Investment and Supplies co.Ltd walipongeza juhudi na ushirikiano wanaopata kwa serikali .
Ernesty alisema ,wameanza uzalishaji mwaka wa pili sasa,kwa siku wanazalisha Tani 40 ambapo wanazalisha mabomba Q2 pipe,bomba kubwa na round pipe.