*******************
18/03/2022 KILIMANJARO
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amewataka askari Polisi kote nchini kuendelea kutumia weledi, maadili na ushirikishwaji wa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Sagini amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa cheo cha Koplo wa Polisi katika Shule ya Polisi iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya askari 1750 wamehitimu mafunzo hayo na kuwaagiza askari hao kwenda kuyashughulikia makosa ya uhalifu wa kimtandao ambapo baadhi yamekuwa yakidhalilisha Utu, Kuchochea chuki na uhasama katika Jamii zetu pamoja na kuathiri uchumi na kutishia amani, utulivu na usalama.
Hata hivyo, Naibu Waziri Sagini ameuagiza Uongozi wa Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kuzuia uhalifu na kuwashughulikia wahalifu wote watakaobainika.