Meneja uhifadhi ,taarifa na uchapishaji kutoka COSTECH ,Dokta Bunini Manyilizu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Arusha .(Happy Lazaro)
Waandishi wa habari pamoja na watafiti kutoka kanda ya kaskazini wakiwa katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia(COSTECH)Happy Lazaro.
**********************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Waandishi wa habari wametakiwa kutumia kalamu zao ipasavyo katika kuandika habari za sayansi na teknolojia ili tafiti zinazofanyika ziweze kuwafikia watumiaji .
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Meneja uhifadhi taarifa na uchapishaji kutoka tume hiyo,Dokta Bunini Manyilizu wakati akizungumza katika ufungaji wa mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti wa kanda ya kaskazini yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia nchini Tanzania (COSTECH).
Amesema kuwa,kuna tafiti nyingi sana ambazo zimekuwa zikifanyika katika maeneo mbalimbali ,ambapo changamoto iliyopo ni tafiti hizo kutowafikia watumiaji ambao ni wananchi kwa wakati
Dokta Manyilizu amesema kuwa,nchi yoyote ili iweze kuendelea ni lazima ijikite katika tafiti kwani tafiti ndizo zinatumika katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii .
“Tuna taarifa nyingi sana kwenye masuala ya sayansi na teknolojia lakini changamoto kubwa iliyopo ni kutopata wadau wa kufikisha taaluma hiyo kwa walengwa na nyie ndio watu pekee mtakaotuwezesha kufikisha taarifa hizo kwa wingi na kwa wakati ili zilete matokeo chanya kwa wananchi.”amesema dokta.
Naye Mkurugenzi wa idara ya menejimenti ya maarifa kutoka COSTECH ,Dokta Philbert Luhunga amesema kuwa,amewataka waandishi wa habari kubadilika na kuwa na nidhamu katika utendaji kazi kwa kuripoti habari zenye kweli ambazo zitaleta tija kwa wananchi na kuchochea mafanikio.
Dokta Luhunga amewataka waandishi hao kupeleka matokeo ya utafiti ili yawafikie wananchi kwani kitendo cha wao kuandika habari hizo za sayansi ni fursa kubwa ya kuibadilisha jamii ili kuleta maendeleo endelevu .
“Unajua tafiti zimekuwa zikifanywa kwa malengo ya kuleta maendeleo endelevu na zinasaidia sana kuleta matokeo chanja kwa wananchi kwa kutumia tafiti hizo .”amesema dokta Luhunga .