Kampuni ya Konnect Tanzania, iliyosajiliwa “Konnect Broadband Tanzania Limited” ni kampuni tanzu ya Eutelsat iliyojitolea kutoa huduma za kasi zaidi za satelaiti.
Kampuni imetangaza kuzindua ofa mpya ya mtandao wa satelaiti nchini Tanzania yenye kasi ya hadi 100Mbps.
Pamoja na leseni zote na kibali cha kiserikali, Konnect Tanzania ina vibali vyote vinavyohitajika ili kuweza kutoa huduma za kimtandao wa bei nafuu nchini.
Kulingana na Utafiti wa Uchumi wa Simu wa GSMA wa 2021, chini ya 28% ya watu katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaweza kupata mtandao wa simu.
Hii inashiria kuwa kuna sehemu nyingine ulimwenguni ufikiaji wake ni wachini kama vile Europe na zaidi ya 80% ya watu wameunganishwa. Uchumi wa intaneti barani Afrika una uwezo wa kufikia dola bilioni 180 ifikapo 2025, ambayo ingewakilisha 5.2% ya Pato la Taifa la bara kupitia kupanua matumizi ya kidijitali, ukuaji wa miji na kupenya kwa simu mahiri.
Utoaji wa huduma za uhakika na haraka kote Tanzania ni muhimu kwa kuzingatia upenyezaji mdogo wa intaneti nchini, iliyo chini ya 20%. Huku muunganisho ukiwa juu zaidi, huduma za mtandao wa Konnect Tanzania, zilizoundwa na kupangwa kwa mahitaji ya ndani, sasa zinapatikana kwa watumiaji wa aina zote nchini kote, kuanzia majumbani na biashara hadi mamlaka za umma.
Meneja Mkuu wa Konnect Bw. Philippe Baudrier alieleza kuwa: “Huduma za mtandao wa Konnect zimeundwa kukidhi mahitaji ya makazi na SMBs (wafanyabiashara wadogo na wa kati) lakini pia zinaweza kusaidia katika maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo, utalii, madini, elimu na afya.
Mtandao wa kasi wa juu ni ufunguo wa kuboresha shughuli za kilimo ambazo zinawakilisha 26,74% ya pato la taifa la Tanzania. Kuongeza tija katika sekta ya kilimo sio tu kukuza Pato la Taifa,bali kutaongeza maendeleo ya taifa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kitaifa wa Kikundi cha Wakulima nchini Tanzania Bw Stephen Ruvuga alisema kuwa: “Mashamba mengi ya kilimo nchini Tanzania yapo katika maeneo yaliyotengwa na hakuna mtandao wa intaneti. Kuunganisha mashamba haya kwa mtandao wa satelaiti kutawawezesha wakulima kukusanya data muhimu kama vile unyevu wa udongo na viwango vya mabwawa, pamoja na ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuboresha ufanisi kwa kasi.
Uwepo wa mtandao wa Kasi katika nyumba za kulala wageni utaongeza usalama na mvuto katika sehemu za kitalii Tanzania, ambao umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la kimataifa na mchango katika Pato la Taifa kushuka kutoka 10.7% mwaka 2019 hadi 5.3% mwaka 2020. .
Upande wake Bw. Kennedy Edward, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Hoteli za HAT Tanzania aliangazia: “Wajasiriamali wa utalii wa Tanzania wanahitaji mtandao wa uhakika ili kutoa huduma bora, kukuza ujuzi, na kufungua masoko mapya.
Kwa vile tovuti nyingi nzuri zaidi za Tanzania ziko katika maeneo ya mbali, Broadband ya satelaiti ya Konnect inaweza kusaidia sekta ya utalii kwa kutoa muunganisho wa intaneti kwa wageni na wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni, zisizoweza kufikiwa na mitandao ya kitamaduni.”
Naibu Mkurugenzi wa chama ya wachimbaji madini Tanzania, Bw. Peter Kabepela, amesema “Kuunganisha migodi ya mbali ya Tanzania kwenye mtandao wa satelaiti kutaongeza tija na kuchangia katika kulinda eneo lao. Pia itaboresha hali ya maisha ya mafundi wanaofanya kazi kwenye maeneo ya uchimbaji madini yaliyo mbali na makazi yao.” Shukrani kwa muunganisho wake wa kasi wa satelaiti, mtandao wa satelaiti wa Konnect ni nyenzo dhabiti katika kusaidia ukuaji wa mchango wa Pato la Taifa wa sekta ya madini kutoka 3,5% hadi 10% ifikapo 2025.