MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Kata ya Makongo, Abbriaty Kivea (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa kata hiyo, Anna Ndemela (wa pili kushoto),alipofika kukagua maendeleo ya mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wajasiriamali inayotolwa na Manispa ya Kinondoni, Dar es Salam, jana.Wa pili kulia ni Katibu wa umoja huo katika kata hiyo, Deodatha Komba na kulia ni Katibu wa UWT wa Tawi la Changanyikeni..
Na CHRISTOPHER LISSA
UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) , Kata ya Makongo, umeanza kufanya tathimini ya kina kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Manispa ya Kinondoni katika kata hiyo.
Akizungumza, Dar es Salam, wakati Kamati ya Utekelezaji ya umoja huo Kata ya Makongo Juu ilipokutana na Ofisa Maendeleo kata hiyo, Mwenyekiti wa UWT wa kata hiyo, Abbriaty Kivea, alisema lengo ni kujiridhisha na maendeleo ya utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo.
“Tunafanya tathimini hii ili kujua ni vikundi vingapi vilipata mikopo, marejesho na changamoto zilizopo ili tuweze kuboresha zaidi na hatimaye mikopo hiyo iwanufaishe walengwa,”anasema Abbriatyy.
Anabainisha , UWT Kata ya Makongo, ina dhamira ya kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia walengwa wengi hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuondoa malalamiko yaliyopo.
“Habari njema ni kwamba, Kata ya Makongo itaanza kutoa mikopo mikubwa zaidi kwa wajasiriamali tofauti na ya awali. Hiyo ni katika kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan. Tutatoa mikopo hiyo kwa vikundi vya watu watano watano,”anaeleza Abbriaty.
Mwenyekiti huyo wa UWT anabainha , tayari vikundi 15 vimejitokeza kuomba mikopo hiyo mikubwa ambapo kikundi kimoja kimeomba kupatiwa sh. milioni 120 kwaajili ya kuendesha mradi wa kilimo cha pilipili.
Anasema kati ya vikundi hivyo kikundi kilichoomba mkopo wa chini zaidi ni sh. milioni 3.5 hali inayoonyesha wazi mikopo hiyo isiyo na riba kuanza kumkomboa mjasiriamali mdogo kuwa mjasiriamali wa kati.
“Kupitia mikopo hii mikubwa wajasiriamali katika Kata ya Makongo Juu wananza kumiliki viwanda .Na hii ndiyo dhamira ya serikali yetu chini ya Rais Samia,”anaeleza.
Abbriaty anasema tathimini hiyo pia ni kutaka kujua mwenendo wa urejeshaji fedha kwa vikundi viliyo kuwa vimekopa ambapo UWT katika kata hiyo ilipokea malalamiko kwa wana vikundi kuwa baadhi vimefanya marejesho lakini havipati mikopo.
“Kuna vikundi ambavyo vimerejesha fedha na kubakiwa na madeni madogo , hivi tunaomba vikopeshwe tena. Visikwamnishwe na watu wachache waliopo ndani ya vikundi hivyo. Pia kuna wengine wanadai wamerejesha fedha lakini wanadaiwa tena,”anasema.
Kwa upande wa Katibu wa UWT wa kata hiyo, Deodatha Kommba, alisema tangu Januari mwaka huu , vikundi 18 vya wajasiriamali vimetambuliwa.
“Vikundi hivi vinaendelea kufanyiwa tathimini, kusajili kisha kupewa mikopo kwani fedha bado zipo,”anaeleza Benadetha.