Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner (kulia) alipomtembelea katika Ofisi yake Jijini Dodoma Machi 16, 2022.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner (kulia) akieleza jambo kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA, Bw. Majaliwa Marwa.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Mwakilishi wa (UNICEF) Bi. Shalini Bahuguna (kushoto) alipomtembelea katika Ofisi yake Jijini Dodoma Machi 16, 2022.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUUN (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………………………………
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner kwa lengo la kushirikiana na Ofisi hiyo katika kuinua na kuimarisha ustawi wa maendeleo ya vijana.
Akizungumza, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Mwakilishi Mkazi huyo kwa kuteuliwa kuongoza shirika hilo la UNFPA nchini.
Aidha, alimshukuru kwa namna Shirika hilo linavyoendelea kuchangia jitihada za Serikali za kuinua na kuimarisha ustawi wa maendeleo ya vijana na Programu ya Stadi za Maisha. Sambamba na hayo alimhakikishia Mwakilishi Mkazi huyo kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha.
Katika wakati mwingine, Waziri Ndalichako amekutana na ugeni kutoka Unicef ukiongozwa na Mwakilishi Bi. Shalini Bahuguna na wamejadiliana mambo mbalimbali ya kushirikiana kati ya ofisi hiyo na shirika hilo la Unicef.