WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dk.Stergomena Tax,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo March 15,2022 jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya Wizara yake katika kipindi cha mwaka mmoja wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia.
……………………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dk.Stergomena Tax ,amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan Wizara yake imepata mafanikio kadhaa ikiwemo kuimarisha ulinzi wa mipaka ya Nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo,Machi 15,2022 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mafanikio hayo,Waziri Stergomena amesema katika kipindi cha mwaka mmoja kupitia JWTZ imeendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka na imeendelea kuwa shwari.
Amesema changamoto chache katika baadhi ya mipaka hususan mpaka wa Kusini changamoto hiyo imeshughulikiwa ipasavyo na hali ya amani na utulivu imeendelea kutamalaki.
Waziri huyo amesema chini ya Serikali ya awamu ya Sita, Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ linavyo vikosi vya Ulinzi wa Amani katika nchi za Lebanon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
“Serikali pia imeendelea kudumisha ushirikiano wa Kimataifa ma Kitaifa katika sekta ya ulinzi hususan kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Afrika (AU) katika operation mbalimbali za ulinzi na amani kwa kupeleka vikosi na usaidizi,waangalizi wa kijeshi,wanadhimu na makamanda katika Nchi zenye migogoro,”amesema.
Waziri huyo amesema katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita , Wizara imewezeshwa kulipa madeni yenye thamani ya zaidi Shilingi billioni 175 kwa Wazabuni waliotoa huduma mbalimbali.
“Hii imejenga imani kwa Serikali na kuiwezesha Wizara kuendesha majukumu yake ya msingi kwa ufanisi,”amesema.
Katika hatua nyingine,Waziri Stergomana amesema mafanikio mengine ya Rais wa awamu ya sita ni pamoja na Ujenzi wa Hospitali ya Jeshi huko Msalato, Jijini Dodoma, kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani.
“Ambapo Uzinduzi wa ujenzi ulifanyika Februari 10 Mwaka huu kwakushirikiana na Nchi ya Ujerumani ambayo imetoa kiasi cha Shilingi bilioni 20 kwaajili ya ujenzi huo,”amesema.
Aidha Wizara, pamoja na Taasisi zilizo chini yake imefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 9,341 kupitia miradi mbalimbali za kudumu na za muda mfupi huku ikifanikiwa kutatua migogoro ya Ardhi74.
“Hospitali hii ni ya hadhi ya Daraja na Nne, pamoja na kutoa huduma kwa wanajeshi na shughuli za jeshi,hospitali hii inategemea kutoa huduma katika ngazi ya Rufaa kwa raia, na hivyo kuongeza uwezo wa kitabibu Jijini Dodoma, na kwa Taifa kiujumla,”amesema.