Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati akifungua Kongamano la wadau katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya haki za mtumiaji Duniani leo hii Jijini Mwanza
Naibu Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT), Dkt. Benard Kibesse akizungumza kwenye Kongamano hilo leo hii Ijumanne Machi 15,2022 katika ukumbi wa Gold crest uliopo Jijini Mwanza
Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) Salma Maghimbi akizungumza kwenye Kongamano
Mwenyeki wa Tume ya Ushindani (FCC), Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumza kwenye Kongamano la maadhimisho ya siku ya haki za kumlinda mtumiaji Duniani katika ukumbi wa Gold crest uliopo Jijini Mwanza
Baadhi ya wadau waliohudhulia kwenye Kongamano lililofanyika leo hii Jijini Mwanza
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi wa pinki)akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohudhulia Kongamano la maadhimisho ya siku ya haki za mtumiaji Duniani.
************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji ameiagiza Tume ya Ushindani (FCC), kufanya Tathimini katika soko ili waweze kubaini mapungufu yaliyopo katika kumlinda mtumiaji sanjari na mtumiaji wa huduma za kifedha ikiwemo huduma za fedha kidigitali.
Maagizo hayo ameyatoa leo hii Ijumanne Machi 15,2022 Jijini Mwanza wakati akifungua Kongamano la wadau katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya haki za mtumiaji Duniani.
Dk.Kijaji amesema kwa kutambua changamoto zinazoambatana na kuunganika na mifumo ya fedha kidigitali,Kama vile tatizo la usalama hafifu wa kimtandao,ipo haja ya kuliangalia eneo hili kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha mtumiaji wa huduma za fedha analindwa dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza sokoni katika miamala na huduma zinazohisisha matumizi ya fedha kidigitali.
Ameongeza kuwa Tume ya Ushindani ifanye Tathimini ya matokeo ya utafiti husika na kuishauri Serikali kuhusiana na mahitaji mapya ya kisera,kisheria,taratibu na kanuni ili kuhakikisha kuwa jukumu la msingi la kumlinda mtumiaji wa Tanzania hususani kwa sekta zisizo chini ya Mamlaka za udhibiti wa kisekta linaboreshwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani (FCC) Dkt. Aggrey Mlimuka amesema kuwa Kongamano hilo ni mwendelezo wa utekelezaji wa jukumu la kupeleka elimu kwa umma kuhusu haki,wajibu na nafuu zinazopatikana kwa watumiaji kupitia sheria namba 8 ya Ushindani ya mwaka 2005.
Dkt Mlimuka ameeleza kuwa Tume hiyo ipo kwenye mchakato wa kurekebisha sheria yake ili kuwezesha kushughulikia masuala ya kumlinda mtumiaji ipasavyo hususani katika kumlinda mtumiaji kidigitali.
“Tanzania tayari tumesha andaa mfumo wa Kitaifa wa kuwainda watumiaji wa huduma za kifedha na nimatumaini yetu kuwa baada ya Kongamano hili watanzania watakuwa wamepata elimu itakayowawezesha kujua haki zao nakuzifuatilia katika kazi zao”,amesema Mlimuka.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT), Salma Maghimbi ametoa wito kwa wanasheria waliohudhulia Kongamano hilo, kutambua kuwa utekelezaji wa sheria ya Ushindani ni fursa muhimu kwao kujifunza zaidi kuhusu kanuni na mbinu za kuendesha mashauri ya Ushindani na kumlinda mlaji ili waweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uwasilishaji wa mashauri.
Awali akizungumza katika Kongamano hilo Naibu Gavana wa Benki Kuu (BOT), Dkt. Benard Kibesse amesema utafiti wa fedha za kidigitali unategemea sana uwepo wa mifumo bora ya kisheria na usimamizi ili kuhakikisha wanakuwa na usawa wa watumiaji wa huduma za kifedha.