Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea eneo la upandaji wa miti katika chanzo cha maji eneo la Mzakwe ambacho ni chanzo muhimu cha maji mkoani Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisisitiza jambo wakati katika eneo la upandaji wa miti katika chanzo cha maji eneo la Mzakwe ambacho ni chanzo muhimu cha maji mkoani Dodoma mara baada ya kutembelea eneo hilo.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt.Fatuma Mganga,akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka akikagua eneo la upandaji wa miti katika chanzo cha maji eneo la Mzakwe ambacho ni chanzo muhimu cha maji mkoani Dodoma mara baada ya kutembelea eneo hilo.
Mstahiki Meya jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe,akielezea umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii ya eneo husika katika utunzaji wa chanzo cha maji eneo la Mzakwe.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimsikiliza Mkazi wa Makutupora Mzee Shaban Nyambo,wakati wa ziara ya kukagua eneo la upandaji wa miti
Muonekano wa chanzo cha maji eneo la Mzakwe ambacho ni chanzo muhimu cha maji mkoani Dodoma.
……………………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAKALA wa Misitu Tanzania (TFS) pamoja na uongozi wa bonde la maji la Wami Ruvu umetakiwa kuongeza jitihada za upandaji na utunzaji wa miti katika chanzo cha maji eneo la Mzakwe jijini Dodoma .
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea eneo la upandaji wa miti katika chanzo hicho cha maji ambacho ni chanzo muhimu cha maji mkoani Dodoma.
Mtaka amesema kuwa haridhishwa na hali ya upandaji wa miti katika eneo hilo lenye zaidi ekari elfu nne ,ikiwa ni sehemu ya ziara yake maalum kuhusu masuala ya utunzaji wa mazingira .
”Nawataka TFS pamoja na uongozi wa bonde la maji la Wami Ruvu muongeze jitihada za upandaji na utunzaji wa miti katika chanzo cha maji hiki ili koundoa hali kama hii”amesema Mtaka
Aidha,Mtaka amesema takwimu zinazotolewa juu ya idadi ya miti iliyopandwa katika eneo hilo haziendani na hali halisi na kuwataka viongozi wa bonde kuacha uzembe na kudanganya viongozi wakuu wa nchi.
RC Mtaka ameagiza sheria zitekelezwe ikiwemo faini ya kuanzia Tsh.50,000 hadi Tsh.300,000 kwa watu watakaokamatwa kwa kuingiza mifugo au kuchoma moto chanzo hicho.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt.Fatuma Mganga amesema kuna umuhimu wa uratibu mzuri wa utunzaji wa miti katika chanzo hicho.
Naye Mstahiki Meya jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe amesema kuwa kuna umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii ya eneo husika katika utunzaji wa chanzo hicho.
Awali Mhifadhi misitu wa wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kanda ya kati Alexanda Mboya ameanisha changamoto zilizosababisha miti iliyopandwa kutostawi katika eneo hilo kuwa ni pamoja na mbuga hivyo mahitaji ya eneo hilo la chanzo cha maji Mzakwe ni miti ya asili.