Na.WAF,Dar es Salaam
Viongozi wa Wizara ya Afya wametakiwa kuwasaidia viongozi wa wizara pamoja na kusimamia sekta ya afya ili isonge mbele.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel wakati akitoa salamu za Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kwenye mafunzo elekezi kwa viongozi kwa wajumbe wa menejimenti wa wizara hiyo
Dkt.Mollel amesema kuwa viongozi hao ni mikono ya Serikali hivyo kila wanachofanya ni kwa lengo la kuisaidia serikali na wananchi wanaohitaji huduma bora za afya
“Sisi ni wizara ya afya na wa mambo magumu tunategemewa kutoa majibu kwa wananchi hivyo ni muhimu kutafakari kwa undani ,hivyo kama viongozi mnapaswa kuwa wabunifu na kuwekeza ili kupata viongozi wengine wazuri na tusiwe watu wa madododso”.
“Sisi tusiwe watu wa kuwekeza kwa wenye akili za kupitiliza yaani ugunduzi tunategemewa kugundua dawa ya Saratani,Corona na mengineyo hilo ndilo wananchi wanategemea na sio kukopi tu elimu za wengine tujiulize nini ubunifu wetu na Waziri Ummy Mwalimu ana ana mategemeo makubwa kwa ninyi wakurugenzi na wakuu wa idara”Aliongeza Dkt. Mollel