Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Zainabu Chaula,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Bw.Lameck Sendo,akizungumzia malengo ya mkutano huo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Bw.Lameck Sendo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Afisa Miradi Mwandamizi kutoka Shirika la Misaada kwa jamii ya Maendeleo Doreen Rutechura,akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya Wazee wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akimsikiliza Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi.Clotilda Kokupima wakati akitoa neno la shukrani mara baada ya kuzinduliwa kwa Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Baraza la Wazee la Taifa leo March 11,2022 jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA
.………………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima,amekemea vikali na kulaani vitendo vya mauaji dhidi ya Wazee ambavyo vimekuwa vikijitokeza kwa tuhuma za ushirikina katika jamii .
Hayo ameyasema leo March 11,2022 jijini Dodoma wakati akizindua wa Baraza la Taifa la Wazee, Dk Gwajima amesema kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kupambana na mauaji jambo ambalo takwimu zinaonesha kuwa yamepungua kutoka wazee 190 mwaka 2015 hadi kufikia wazee 54 mwaka 2020.
“ Takwimu hizi hazinifurahishi, watu 54 bado ni watu wengi, hii kuendelea na mauaji ya wazee kwa kisingizi za uchawi kutokana na kuwa na macho mekundu, huu uchawi wanauonana wao tu, ni lazima tuikomeshe hali hii na tutashuka hadi chini kwa kushirikiana na jamii na viongozi wa dini.”
Aidha Dkt Gwajima ameainisha juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ikiwemo kusimamia upatikanaji wa huduma kwa kuwapatia vitambulisho vitavyowawezesha wao kupata huduma za afya bure katika Vituo vya Afya nchini.
“Hadi sasa jumla ya wazee 1, 256 ,544 wameshapata vitambulisho vya kupata huduma ya Afya pamoja na Madirisha 2,335 ya kutolea huduma katika vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini” alisema Dkt Gwajima.
Aidha Dk.Gwajima ameisihi jamii kuwajibika katika kuwajali, kuwatunza wazee ili wasikose matunzo na baadhi kugeuka kuwa ombaomba katika baadhi ya maeneo nchini.
Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema Serikali imejipanga katika kuboresha makazi ya wazee kwa kukarabati na kujenga miundombinu mipya katika makazi hayo ili waweze kupata huduma Bora “alisema Dkt Gwajima.
Dk Gwajima amesema kuwa Wizara ipo katika hatua za kuhuisha Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na kuanza mchakato wa utungaji wa Sheria ya Wazee.
“Kukamilishwa kwa nyaraka hizi kutaboresha maslahi zaidi ya wazee katika ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Dk Gwajima ametoa rai kwa wajumbe wa Baraza hilo kutumia ujuzi na uzoefu walionao na kwa weledi mkubwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili wazee na kusaidia wazee kutumia fursa zilizopo ndani ya jamii kuimarisha ustawi na maendeleo yao.
“ Niwaase tusitumie Baraza hili kama jukwaa la harakati, bali kiwe ni chombo cha kuishauri serikali katika kuleta maendeleo kwa nchi yetu.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewasisitiza wazee kushiriki kikamilifu katika kuwalea vijana wao ili kupata jamii yenye maadili na uzalendo kwa Taifa.
“Wengine tumesomeshwa na Serikali,tuna kazi ya kuhakikisha vijana wetu ambao ni wazee watarajiwa wasimamishwe na waweze kustawi” amesema Dkt. Chaula
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi.Clotilda Kokupima ameishukuru Serikali kwa uundwaji wa Baraza hilo na kuomba liimarishwe ili liweze kufanya kazi iliyokusudiwa kwa kuwaunganisha Wazee kujadili changamoto zao ili wapate ufumbuzi wa changamoto hizo kutoka kwa Serikali na wadau mbalimbali.
“Mabaraza hayo yameundwa kwa waraka kutoka ofisi ya Waziri Mkuu ambapo Mikoa takribani yote imeweza kupata wawakilishi wao ili kupata mawazo na maoni ya kuboresha masuala mbalimbali ya Wazee nchini “ amesema Clotilda
Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Wazee, Lameck Sendo amesema kuwa uundwaji wa baraza hilo utaleta heshima kubwa kwa wazee na jamii itawadhamini na kuwatunza.
‘Ombi langu kwa Wizara ihakikishe inakamilisha utungwaji wa sheria hasa kutokana na kuwapo sera ya wazee kwa muda mrefu bila kuwapo sheria.’amesema Bw.Sendo