Eng.Jane Kadoda (Afisa Mazingira Mwandamizi) akitoa elimu juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NEMC kwenye maonesho Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini QatarMeneja Kanda ya Ziwa Victoria Bw.Jarome Kayombo wakipadilishana uzoefu na technolojia ya uhifadhi wa taka zitokanazo na mabaki ya chakula ( food waste) kwenda kutengeneza mbolea. Ameahidi kushirikiana na NEMC kwa kuleta technolojia hiyo mbadala nchini TanzaniaEng.Jane Kadoda (Afisa Mazingira Mwandamizi) akitoa elimu juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NEMC kwenye maonesho Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini QatarWashiriki kutoka NEMC wakijadili baadhi ya maoni/mapendekezo yaliyotolewa na washiriki mbalimbali waliotembea banda la NEMC nchini Qatar
***********************
Tanzania ni miongoni mwa Nchi 130 zilizoweza kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira ambayo huwa yanafanyika kila mwaka na kwa mwaka huu yanafanyika kuanzia tarehe 10 hadi 14 Machi, 2022 katika jiji la Doha Nchini Qatar.
Aidha maonesho haya yamejumuisha Makampuni ya Kimataifa 300, Wakulima 100 pamoja na wawasilisha Mada wapatao 56 kutoka Mataifa mbalimbali.
Maonesho yalifunguliwa tarehe 10 Machi, 2022 na Waziri wa Wizara ya Manispaa na Mazingira ( Ministry of Municipality and Environment) Mhe. Abdulla bin Abdulaziz bin Turki Al Subaiel.
Lengo kuu la maonesho haya ni kutoa fursa kwa washiriki kuonyesha bidhaa na huduma zinazohusiana na kilimo na mazingira.
Pia maonesho haya yanawapa fursa washiriki kubadilishana uzoefu, technologia pamoja kutafuta masoko na fursa na uwekezaji katika kilimo na usimamizi wa mazingira.
Baraza la Taifa la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni miongoni mwa Taasisi kumi na tisa (19) zilizoshiriki kutoka Tanzania.
Tanzania tulikuwa na jumla ya mabanda 19 ambapo kati yake 17 ni kutoka taasisi za Serikali zinazoshughulika na Mazingira, Kilimo, Ufugaji na Uwekezaji.
Baadhi ya taasisi za Serikali ni pamoja na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania -Qatar, NEMC, TIC, Bodi ya Korosho, Bodi ya Maziwa, Bodi ya Chai, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanyangiko pamoja na Umoja wa kilimo cha mbogamboga.
Washiriki wengine kutoka Tanzania ni pamoja na MamboJambo Design, Dumas African, Greencom African Ltd, Natural Shine Traders na Kampuni ya Oasisi Import Export Ltd.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira liliwakilishwa na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Bi. Irene John, Meneja wa Kanda ya Ziwa; Bw. Jarome Kayombo pamoja na Mha. Jane Kadoda kutoka Kanda ya Morogoro Rufiji.
Miongoni mwa wageni waliotembelea banda la NEMC siku ya ufunguzi ni pamoja na balozi wa Tanzania nchini Qatar Mh. Balozi Mahadhi Juma, Barozi wa Burundi – Qatar, taasisi za Serikali, Wizara na Kampuni mbalimbali kutoka nchi washiriki kama vile Wizara ya Manispaa na Mazingira, Kitengo cha Hifadhi ya Bahari wakiwakilishwa na Prof. John Man Kon Wong, Kampuni ya CITC wanaojihusisha na ufungaji mitambo ya kupunguza hewa ukaa kwenye magari, Techkinologia ya kuongeza tija kwenye kilimo na mazingira.
Kampuni ya Royal Link hawa wanajihusisha na Uzalishaji na Usambazaji wa Chemikali za Viwandani, Kampuni za kusafisha maji taka na maji ya Bahari.
Aidha, mwananchi mmoja mmoja kutoka Qatar na nchi mbalimbali walitembelea banda la NEMC ili kupata elimu pamoja ma kuelezwa fursa za uwekezaji kwenye mazingira, utalii na kilimo.
Akizungumza katika maonesho hayo ; Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Irene John amesema maonesho hayo yatafungua fursa nyingi za uwekezaji katika bidhaa na huduma kwani kupitia mawasilisho yaliyofanywa siku ya ufunguzi tarehe 10 Machi, 2022 NEMC imeonesha jinsi gani mazingira ya uwekezaji yameboreshwa kupitia mifumo mbalimbali ya kielektronic kama vile mchakato wa utoaji vibali vya Tathimini ya Athari kwa Mazingira ( TAM) na pia mfumo wa upatikanaji wa vibali vya taka hatarishi ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika.
Kupitia Meneja wa Kanda ya Ziwa Bw. Jarome Kayombo amebainisha kuwa moja ya faida kubwa kwa NEMC kushiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Mazingira na Kilimo ni pamoja na kuitangaza NEMC na pia kutoa elimu juu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa uwekezaji endelevu.
Aidha, maonesho yametoa fursa ya fursa za uwekezaji na kuelemisha washiriki juu ya mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira Nchini Tanzania.
Pia maonesho haya yametoa fursa ya kubadilishana uzoefu wa technologia mbadala za kutunza mazingira zitakazoleta tija katika kuboresha maisha ya kila siku.