Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli akikabidhi vyeti kwa Wahitimu wa mafuzo mafupi Chuoni TaSUBa, Mahafali yamefanyika leo Bagamoyo mkoani Pwani Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa mafuzo mafupi Chuoni TaSUBa, Mahafali yamefanyika leo Bagamoyo mkoani PwaniTaasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa mafuzo mafupi Chuoni TaSUBa, Mahafali yamefanyika leo Bagamoyo mkoani Pwani. Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango fedha na Utawala Emmanuel Bwire akizungumza kwenye mahafali ya Wahitimu wa mafuzo mafupi Chuoni TaSUBa, Mahafali yamefanyika leo Bagamoyo mkoani Pwani Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli akipata picha ya pamoja na baadhi wa Wahitimu wa mafuzo mafupi Chuoni TaSUBa, Mahafali yamefanyika leo Bagamoyo mkoani Pwani
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo mafupi Chuo cha TaSUBa wakitoa burudani kwenye mahafali ya wahitimu hao yaliyofanyika leo Bagamoyo Mkoani Pwani.
********************
NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO
Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli ameipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) kwa kuendelea kuibua vipaji vya vijana wakitanzania kupitia sanaa mbalimbali.
Bw.Kaziyareli ametoa pongezi hizo leo wakati akisoma hotuba kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika Mahafali ya wahitimu wa Mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha TaSUBa ambao wamefadhiriwa na wafadhiri mbalimbali.
Amesema kuna umuhimu wa wahitimu kuhakikisha wanazitafuta fursa kupitia mafunzo waliyoyapata na wasisubiri fursa ziwafuate.
Nae Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye amesema kampuni ya TTC imekuwa ikidhamini vijana kupata mafunzo ya sanaa katika Chuo hicho tokea mwaka 2017 na vijana hao wanahitimu wakiwa wamejengeka.
“Wahitimu wanaohitimu leo ni Vijana waliofadhiriwa na Taasisi ya TULIA TRUST vijana 25 na wengine wamefadhiriwa na Kampuni ya MUSICIAN FOR BETTER LIFE vijana 58”. Amesema Dkt.Makoye.
Aidha Dkt.Makoye amewataka wahitimu kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao watahitaji kujiunga na Chuo hicho ili nao waweze kukuza vipaji vyao.
Kwa upande wake mwakilishi wa Wahitimu wa mafunzo akitoa risala mbele ya Mgeni rasmi, Martine Mwangomale amesema kupitia mafunzo walioyapata ya muda mfupi yamewasaidia kuongeza ujuzi na maarifa katika Sanaa ambayo wamekuwa wakiifanya Pia wameweza kushirikiana na kubadilishana mawazo baina yao na Walimu waliokuwa wakiwafundisha Chuoni hapo.
Amesema muda wa kushiriki mafunzo hayo yalikuwa ni mafupi hivyo wameomba Kwa wakati mwingine mafunzo kama hayo yatolewa Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Pamoja na hayo wamewashukuru walimu kwa kutoa ushirikiano wa kutosha toka walipofika chuoni hapo na kuanza mafunzo kwani ushirikiano huwa umewajengea uelewa mkubwa kupitia mafunzo hayo.
“Tunamshukuru mama yetu Dkt.Tulia Ackson Mwansasu Kwa kutupatia fursa hii nzuri ya kuendeleza vipaji vyetu katika Sanaa”. Amesema Mwangomale.