Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), wakati wa Mkutano wa Wabunge wote kuhusu uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022 – 2023 uliofanyika leo Machi 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akishiriki katika Mkutano wa Wabunge wote kuhusu uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022 – 2023 uliofanyika leo Machi 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022 – 2023 mbele ya Waheshimiwa Wabunge katika Mkutano uliofanyika leo Machi 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akitoa maneno ya utangulizi mbele ya Wabunge na Watendaji wa Serikali (Wizara ya Fedha na Mipango) wakati wa Mkutano wa Wabunge wote kuhusu uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022 – 2023 uliofanyika leo Machi 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu (Mb)
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika Mkutano kuhusu uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022 – 2023 uliofanyika leo Machi 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)