Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipowasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia jijini Riyadh na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi huo.
Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kulia) wakiangalia picha ukutani (hazipo ktika picha) walipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh kwa ajili ya kukagua ubalozi huo na kuzungumza na watumishi.
Balozi Liberata Mulamula (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (wa kwanza kulia) huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (kushoto) akifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kulia) akiwaonesha kitu Balozi Liberata Mulamula (katikati) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) walipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh .
Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia walipotembelea Ofisi hizi jijini Riyadh .
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh.
kikao kikiendelea katika Ofisi za Ubalozi jijini Riyadh
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh.

*****************
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia nchini humo.
Akizungumza na Watumishi wa Ubalozi jijini Riyadh, Balozi Mulamula amewataka kuzingatia ulinzi wa taswira ya nchi yao hasa kwa kuzingatia mienendo ya maisha yao na kauli zao pia.
“Chochote mnachofanya ndio sura na kioo cha Jamhui ya Muungano wa Tanzania huku, nawaombeni sana kuzingatia hilo, japo ni kweli kwa mienendo yenu hatuwaingilii lakini hamna budi kujua kuwa nyie ni taswira ya nchi yetu huku,” alisema Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanafuata na kuzingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma licha ya kutekeleza majukumu yao nje ya Tanzania.
Pia amewataka Mabalozi na watumishi walioko katika balozi za Tanzania kuendela kuwa walezi wa Watanzania popote walipo na kuwa tayari kuwasaidia pale watakapohitaji msaada kutoka katika balozi hizo.
Waziri Mulamula yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alioutoa mwezi Machi 2021 alipotembelea Tanzania na anataarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.
Katika ziara hiyo Waziri Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki , kituo cha Uwekezaji nchini na Chama cha cha wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA)

********************