Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akizungumza na wanasheria wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) mara baada ya kutembelea taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Taasisi Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam.Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Machapisho, Law Shool Prof.Zakayo Lukumay akieleza jambo mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene pamoja Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud mara baada ya waziri huyo kufanya ziara kwenye taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene mara baada ya kufanya ziara kwenye taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geofrey Pinda (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akipokelewa na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Dkt. Benhajj Masoud pamoja na watumishi wa taasisi hiyo kufanya ziara kwenye Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akipokelewa na watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geofrey Pinda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) akiongozana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene kufanya ziara kwenye taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akimsikiliza Mkutubi Msaidizi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Bi.Nyabwile Mganga mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akimsikiliza Mkutubi Mwandamizi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Bi.Bahati Mugini mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akimsikiliza Mkutubi Msaidizi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Bi.Nyabwile Mganga mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene amesema kuwa anaridhishwa kwa kasi kubwa na taaluma inayotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini katika kuwaanda wanasheria huku akiweka wazi mipango ya Serikali kuendelea kukijengea uwezo wa kifedha chuo hicho ili kiweze kuongeza ufanisi.
Waziri Simbachawene ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara yake ya kikazi katika Taasisi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema jukumu lililopewa Chuo hicho na Serikali kuwaandaa wanasheria kwa ajili ya kuisadia shughuli zake katika masuala mbalimbali ya kisheria linatimizwa kwa vitendo kutokana na matokeo inayoyaona.
“Nimejifunza mambo mengi nilipofika hapa, kwanza ni mgawanyo wa masomo wanayoyatumia katika kuwaandaa wanafunzi, lakini namna mahakama za mfano zinavyoendeshwa mahali hapa, kimsingi hapa wanafanya mambo yanayotokea kabisa mahakamani jambo linalonipa imani kuwa kuwa ile kazi ambayo Serikali tulikusudia ya kuwaanda mawakili wa kushindana na mawakili wengine dunia linatimia” amesema Waziri Simbachawene.
Amesema siku hizi Dunia inaishi katika mikataba na makubaliano ya aina mbalimbali hivyo unapokuwa na wanasheria wazalendo ambao wameandaliwa vizuri ni sawa na kuwa umetengeneza wanajeshi vizuri wa kupambana katika vita yoyote huku akiwataka wanafunzi wanaopata fursa ya kwenda kusoma mahali hapo kuhakikisha wanaweka mkazo katika masomo yao.
Aidha alisema malalamiko ya baadhi ya watu kuhusu idadi ndogo ya wanafunzi wanaohitimu mahali hapo, alisema jukumu la chuo hicho siyo kumuwezesha mwanafunzi kufaulu katika mitihani bali suala la muhimu ni mhitimu kumaliza masomo yake akiwa ameiva kivitendo ili anapokwenda mahakamani aweze kutoa ushindani unaohitajika.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud amesema kimsingi wamefarijika na ziara ya Waziri huyo chuoni hapo kwa kuwa imewaongezea hamasa katika masuala mbalimbali.
Aidha amesema Chuo hicho kitaendelea kutimiza majukumu yake hasa katika kuhakikisha wahitimu wanaotoka mahali hapo wanakuwa na weledi wa kutosha.
Ameeleza kuwa katika kutimiza majukumu yake, taasisi hiyo ambayo ndiyo yenye jukumu kuu la kuwaandaa mawakili nchini, imekuwa ikisimamia suala zima la uelewa wa namna ya kuendesha kesi na usimamizi wa mikataba mbalimbali kwa wanafunzi hao na kusisitiza kuwa nia ni kuisaidia Serikali katika kujenga ustawi imara.