Mdau wa Maendeleo hapa nchini Dk.John Lucian atakuwepo kwenye kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale, Arusha.
UMOJA WA WANAMUZIKITanzania (TAMUFO) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wanatarajia kufanya kongamano kubwa la fursa.
Akizungumza nawaandishi wa habari mjini hapa Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisemakongamalo hilo linalojulikana kama Kongamano la Fursa na Uhamasishaji wa
Utamaduni wa Mtanzania.
Alisema kongamano hilolitakalofanyika Machi 26, 2022 wilayani Karatu mkoani Arusha litaenda sambamba
na kutembelea Mbuga ya Wanyama ya Ziwa Manyara.
Alisema mgeni rasmianatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul.
Aliwataja wanamuziki watakaotoa burudani kuwa ni Mwanamuziki nguli wa kizazi kipya Stara Thomaskutoka Dar es Salaam ambaye ataongoza msafara wa kwenda kufanya utalii wa ndaniZiwa Manyara.
Alitaka mwanamuzikimwingine kuwa ni Hafsa Kazinja ambaye amejiandaa vizuri kutoa burudani safi
siku hiyo ya kongamano hilo.
Alisema wahusika wotewatakutana Karatu ambako kutakuwa na mambo lukuki huku zikipatikana fursambalimbali kama za Bima ya Afya ya NHIF sanjari na kupatiwaelimu kutoka kwa wadau wa maendeleo ambazo zitatolewa kwa wanamuziki na wanajamii
kwa ujumla.
Joel alisema Baraza laSanaa Tanzania ( BASATA) na Chama cha Hatimiliki Tanzania (COSOTA) watakuwepo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu utolewaji wa mirahaba nausajili wa wasanii.
Alisema Watu waMakumbusho ya Taifa pia watakuwepo na watatoa elimu ya uhifadhi wa Utamaduni waMtanzania na Uanzishwaji wa Makumbusho mbalimbali zikiwamo za Wanamuziki.
” Kongamano lanamna hii halijawahi kutokea ni la mara ya kwanza kabisa katika historia yanchi yetu” alisema Joel ambapo alitumia nafasi hiyo kuwakaribishawananchi na wadau mbalimbali wakiwepo wanamuziki na kwa mawasiliano zaidi ya kujuakongamano hilo unaweza kupiga Simu namba 0756846166 au
0712781171.