Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akizungumza wakati akielezea mafanikio ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akisisita jambo wakati akielezea mafanikio ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu), Prof. Caroline Nombo akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara hiyo ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita. Mkurugenzi wa Raslimaliwatu na Utawala wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw.Moshi Kabengwe akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara hiyo ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Bugwesa Katale akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita. Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita. Mkurugenzi wa Taasjsi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wakati Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akipata picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati akielezea mafanikio ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akipata picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo wakati akielezea mafanikio ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
Serikali ya Awamu ya Sita imetoa kipaumbele katika Sekta ya Elimu kwa kuhakikisha mindombinu ya shule za msingi na sekondari imeboreshwa ili kila mtoto wa Kitanzania apewe nafasi ya kupatiwa elimu bora na ya uhakika.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani mbele ya wadau mbalimbali wa elimu amesema, kumekuwa magaeuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini katika huu mwaka mmoja.
Waziri Mkenda amesema kumekuwa na msukumo mkubwa kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule kitu ambacho kimeongeza idadi ya watoto wanaojiunga na masomo kwa shule za Sekondari ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi laki Tisa wamejiunga na kidato cha kwanza.
“Ningependa niliseme jambo hili kwa sababu si wote mtaliangalia kwa jicho hili, Rais wetu, Samia Suluhu Hassan amechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kila mtoto anaenda shule, uwekezaji alioufanya umetuwezesha kuchukua wanafunzi zaidi ya laki Tisa kwa mkupuo kuingia kidato cha kwanza”, alisema Prof. Mkenda.
Aidha amesema amepokea maagizo kutoka kwa Rais Samia mara kadhaa yanayomtaka kuhakikisha watoto wote hata wale walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwepo kupata mimba, watafutiwe mkakati wa namna ya kurudi shule.
Amesema katika kuhakikisha miundombinu ya shule inaandaliwa kupokea idadi kubwa ya wanafunzi kwa mwaka huu, sekta ya elimu imepokea robo ya mgawanyo wa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO – 19 ambapo jumla ya madarasa 15,000 yamejengwa kutokana na fedha hizo.
Ameeleza kuwa kwa upande wa elimu ya juu, ndani ya mwaka mmoja fedha za mikopo zimeongezwa kutoka Bil 464 hadi 570 na kuagiza asilimia sita (6%) iliyokuwa inatozwa kwa ajili ya kulinda thamani ya hela iondolewe na asilimia kumi (10%) kama adhabu ya kuchelewa kulipa ifutwe hii inapelekea wanafunzi wengi kusoma bila kikwazo.
“Kwenye bajeti ya Wizara ya Elimu mwaka huu, tumeongezewa fedha ambazo zimetuwezesha kuchapisha vitabu maalumu ambapo jumla ya vitabu 9,178 kwa ajili ya wanafunzi 353 wasioona na 93,366 kwaajili ya wanafunzi 3,591 wenye uoni hafufi vilivyogharimu shilingi mil 770, lakini pia kuna shule zimejengwa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kama vile Lukuledi- Masasi, Patandi – Arusha na shule zingine zote tuna mwongozo unaohakikisha tunatoa huduma”. Amesema
Prof. Mkenda ametoa rai kwa Watanzania wote wenye watoto ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali kutowafungia ndani bali watumie fursa za elimu ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya watoto wote.