Wawasilishaji wa mada kwenye mjadala katika hafla hiyo akiwemo Dkt Harun Makandi kutoka COSTECH (kulia),Shukuru Nyagawa kutoka E-Link Consult (wa kwanza kulia) na Dr Magreth Samiji kutoka UDSM ( wa pili kulia).
Mtaalamu wa Mazingira na Jinsia kutoka Shirika la E-Link Consult Shukuru Nyagawa akiwasilisha mada ya namna ya mabadiliko ya tabia nchi yanavyoleta changamoto kwa wanawake.
Dr Magreth Samiji kutoka UDSM akiwasilisha mada kwenye mdahalo wa siku ya wanawake kuhusu namna wanavyoweza kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi katika shughuli zao za kila siku.
Washiriki ambao wameshiriki kwenye mdahalo wa siku ya wanawake kuhusu namna wanavyoweza kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi katika shughuli zao za kila siku ambao umefanyika katika ukumbi wa COSTECH.
Picha ya pamoja (picha na Mussa Khalid)
…………………….
NA MUSSA KHALID
Wanawake nchini wametakiwa kutumia teknolojia mbalimbali kuweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi kwa kubadilisha mtindo wa zamani hususani katika kilimo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sanyansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Filbert Luhunga wakati akizungumza kwenye mdahalo wa siku ya wanawake kuhusu namna wanavyoweza kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi katika shughuli zao za kila siku.
Dkt Luhunga amesema kunapotokea mabadiliko ya Tabia nchi waathirika wengi ni wanawake kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupata mahitaji ambayo walikua wakiyapata ikiwemo maji na nishati ya kupikia.
‘Kwenye mdahalo huo tumeona ni kwa jinsi gani mwanamke anavyoathirika kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi hivyo wanajaribu kujadili namna gani watapambana na mabadiliko hayo hivyo ushauri wangu kwa kina mama nikutumia teknolojia mbalimbali kuweza kupambana na mabadiliko’amesema Dkt Luhunga
Aidha amesema ni vyema wakajaribu kubadilisha mtindo wa zamani wa kulijma ikiwa ni pamoja na kutumia pembejeo za kilimo kulima na kutumia teknolojia za nishati mbadala.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Mazingira na Jinsia kutoka Shirika la E-Link Consult Shukuru Nyagawa amewasilisha mada ya namna ya mabadiliko ya tabia nchi yanavyoleta changamoto kwa wanawake ambapo amesema tafiti zinaonyesha kuwa wanawake ndio waathirika zaidi kwa sababu ndio wanategemewa kwenye jamii.
Nao baadhi ya washiriki katika mdahalo huo kutoka COSTECH akiwemo Aisha Mgaya pamoja na Sarah Kabigi wamewashauri wanawake wasibaki nyuma pindi fursa zinapojitokeza ili waweze kuongeza ubunifu katika maendeleo endelevu.
Mdahalo huo ambao umewashirikisha wadau kutoka katika taasisi na maeneo mbalimbali umekwenda sambamba na Dhima ya Usawa a Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu kwa taifa.