Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mashimba Ndaki akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio ya Wizara hiyo ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mashimba Ndaki akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio ya Wizara hiyo ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.
******************
Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mashimba Ndaki amesema Sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini sasa imepiga hatua na kujikita kibiashara zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, Waziri Ndaki alisema soko la nyama na bidhaa za viumbe maji limeongezeka na linatarajiwa kuongezeka zaidi.
“ Katika kuwaunga mkono wafugaji wa mifugo na wavuvi Serikali imehakikisha wadau wa sekta hii wanaunganishwa na Tasisi za fedha, sasa wanaweza kupokea mikopo kama ilivyo kwa sekta nyingine na baadae wakarejesha ili kupata mitaji lakini kwa wale wabunifu wa huduma mbalimbali tunawasaidia kwa kuwatangaza kwa wananchi wanoahitaji huduma zao ili kujipatia kipato” alisema Waziri Mashimba.
Waziri Mashimba alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza Tanzania kwenye masoko ya kimataifa ikiwa ni pamoja na fursa zilizopo jambo lililopelekea kuongezeka maradufu kwa soko la nyama ndani na nje ya nchi.
“ Ndani ya huu mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani, tulipata wageni kadhaa kutoka Nchi za Kiarabu, waliotembelea viwanda vyetu ili kujifunza pamoja na kupata uhakika wa ubora wa mazao ya nyama yanayopatikana”
Aliongeza kwamba baada ya ugeni huo soko la nyama Nchini limeongezeka na linategemewa kuongezeka zaidi kwani ubora wa mazao ya nyama unaozalishwa unakubalika katika masoko ya kimataifa ambapo kuanzia Julai mpaka Januari mwaka huu kilo zipatazo 5000 zimeuzwa, ambapo awali ziliuzwa kilo 1777 tu.
Akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua sababu za kuongezeka kwa bei nyama nchini Waziri ndaki alifafanua kwamba ongezeko hilo la uhitahi ndio lililopelekea kupanda kwa bei ya nyama nchini, lakini pia Serikali inajizuia kuingilia bei ya bidhaa hiyo ili kuruhusu hali ya soko ijiendeshe kadiri ya mahitaji.
Kwa upande wa viumbe maji, Waziri ndaki alisema kwamba Wananchi Mil 4.5 wanakadiriwa kupata kipato chao cha kila siku kutoka kwenye mnyororo wa thamani wa uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji.