Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo akifungua Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) Bi.Mercy Sila akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo akitembelea mabanda ya wajasiriamali Wanawake katika Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
9PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amepongeza maonyesho ya wafanyabiashara wanawake yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini humo ambapo maonesho hayo yameandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC).
Akizungumza wakati akifungua Maonesho hayo Waziri Jafo amesema wanawake wameonesho ujasiri mkubwa kuanzisha vikundi vya uzalishaji wa bidhaa ambazo zinakidhi viwango hali ambayo inachangia upatikanaji wa ajira kwa vijana wa kitanzania.
“Nimefurahi kuona bidhaa zenye hali yya juu tena zinazozalishwa na wanawake wakitanzania, bidhaa ambazo zinakidhi viwango na ubora unaotakiwa nikimaanisha zina nembo ya ubora wa Shirika la Viwango Tanzania”. Amesema Waziri Jafo.
Kwa upande wake Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) Bi.Mercy Silla amesema katika kuhakikisha viwanda vinakuwa nchini watahakikisha kuwahamasisha wanawake wenye viwanda wana kuwa na vyeti vya mazingira ili biashara zao ziweze kukua kupitia viwanda vyao.
Amesema kupitia kauli ya Waziri Jafo wanawake wasibweteke na kuweza kuleta maendeleo zaidi hivyo wao watahakikisha wanashirikiana kuhakikisha wanazidi kuinua uchumi wa nchi kupitia viwanda vyao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Bi. Mwajuma Hamza amesema kupitia maonesho hayo wanapata fursa ya kujitathimini wao kama taasisi ni wapi wamefikia katika kuwezesha wanawake lakini na namna gani wanaweza kuweka mikakati ya kuendelea kuwawezesha wanawake.