Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyabiashara ambaye alifika kwenye banda la BRELA kupatiwa huduma kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Brela pamoja na wateja mara baada ya kutembelea banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
*****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewapongeza Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa kuendelea kutoa elimu ya kwa wafanyabiashara kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la BRELA kwenye viwanja hivyo Waziri Jafo amesema uwepo wa Wakala hao katika maonesho hayo kutawarahisisha wajasiriamali wanawake kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu kuhusu umuhimu wa kusajili biashara zao na kupata vyeti.
Amesema suala la kusajili biashara kwa wajasiriamali ni muhimu hasa katika masuala ya biashara, hivyo kupitia maonesho hayo yatawajengea uelewa mkubwa wajasiriamali namna watakavyoona umuhimu wa kusajili biashara zao.